Kudidimia kwa Elimu - Serikali Yakacha Kuchunguzwa na Bunge

Richard Mlangi

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2012
Posts
380
Reaction score
193
Hoja ya Mh. Mbatia ilikuwa imesimama hasa ukizingatia hali mbaya ya elimu inayolikabili taifa letu.
Mh. Mbatia alitaka iundwe tume ya Bunge kuchunguza sababu za kuanguka kwa elimu nchini na kutoa maelekezo kwa serikali ya hatua za kuchukua kunusuru hali hiyo.
Hata hivyo, kama ilivyo kawaida yake, Spika mara nyingi huegemea upande wa serikali, ...hoja hiyo haikupita.
Kuna madudu mengi sana katika sekta ya elimu, ila kwa mfumo huu wa Bunge letu ambalo linasimamiwa na serikali badala ya kuisimamia serikali, ...hatufiki popote !
 
Isitoshe maamuzi ya wabunge hufanywa kivyama. Ndiyo maana maamuzi ya wana-ccm hupita nyakati zote. Hoja za upinzani hata kama zinafaa hupondwa.
 
Ya leo kali zaidi Ukada ni aibu
Wana jamvi najitokeza kutoa hoja hii juu ya umbumbumbu mkubwa uliooneshwa na ukada na ushabiki wa kizembe uliooneshwa na bunge letu hii leo asubuhi, wakati Mheshimiwa James Mbatia akitakiwa kuhitimisha hoja yake binafsi juu ya Udhaifu mkubwa uliopo katika sekta ya elimu nchini. Mheshimiwa James Mbatia kwa taarifa yake ametumia miaka kumi na nane kufanya utafiti na kuibuka na hoja hii binafsi, lakini cha kusikitisha hoja na utafiti wake vimepuuzwa na naibu spika Ndugai. Hii imethibitisha wazi kwamba nchi hii inaendeshwa bila kuwa na MTAALA RASMI kama alivyosema Mheshimiwa Mbatia kwa miaka yote hii. Taarifa za uhakika ni kwamba Mitaala rasmi ya mwaka 2005 iko katika hatua ya rasimu ambayo ilichapishwa mwaka 2012 yaani mwaka jana kwa maana hiyo kile ambacho waziri wa elimu anakiita mitaala rasmi ni rasimu ya mitaala hiyo na si mitaala yenyewe. Kwa kuanzia sharti tujiulize maswali haya; Hivi Elimu ya nchi hii tunaipeleka wapi (Waziri wz Elimu na Watendaji wake)? Hoja nzuri na ya msingi kama ya Mheshimiwa James Mbatia ni halali kuhitimishwa kiuzembe namna ile? Kwa nini waziri wa elimu hajalieleza bunge ukweli kuwa kilichopo ni rasimu ya Mitaala rasmi na si mitaala kamili? Hivi ni kweli nchi hii haina mitaala rasmi, kama ipo kwa nini wanaweka siri kubwa juu yake kwani kuna uozo gani huko kwenye hiyo mitaala? Hivi kuna ugumu gani uliomfanya waziri wa elimu kushindwa kuwasilisha mitaala hiyo bungeni kama alivyoahidi katika bunge lililopita? Kwa nini waziri ameshindwa kumkabidhi mtoa hoja japo ile mitaala miwili anayoionesha bungeni au hata kumkabidhi Naibu Spika au alishika vitabu vyake vya hadithi na kuvionesha juu kumbe si mitaala? Kama wanayo hiyo mitaala rasmi kwa nini wamegwaya kuileta bungeni tangu mwaka jana na wanaendelea kutoa ahadi kwamba italetwa kabla ya kabla ya bunge kuahirishwa tarehe 8? Kama waliahidi, hawajatekeleza tuwaamini vipi kwamba wataleta hiyo mitaala kabla ya tarehe 8/2/2013? Je, ahadi zao za Kijuha kama hizi wataendelea nazo mpaka lini kwani hata mheshimiwa rais JK mwenyewe ameingia katika ahadi hewa kwamba walimu wataajiriwa tarehe 13/01/2013 ahadi ambaya haijatekelezwa hadi leo au alimaanisha tarehe hiyo ya mwaka 2014? Uongo na uzembe huu mwisho wake lini? Hii nchi ni bora ya Giningi, Kusadikika na Kufikirika. Haya yanayoendelea ya kukumbatia uozo ni aibu kubwa na bomu lililolipuka tayari kwa matokeo mabovu katika mitihani yooote ya taifa.
 
sera na mifumo mibovu ya kisiasa nchini ndo chanzo na mzizi mkubwa wa matatizo haya yote. taifa kutokua na kauli moja imeletwa na mitizamo hasi ya sera ya vyama vingi ambapo sasa wanasiasa wanakumbatia uvyama na si utaifa. hiyo inajidhihirisha sana na haitofutika katika kila maswala hasa yanayohitaji maamuzi bungeni. swala la msingi ni kubadili mifumo ambayo inapelekea kutokua na kauli ya pamoja hasa ktk maswala yanayohitaji maamuzi ya pamoja.
 
Elimu ya kata inatoa wahitimu kata. Mwenye macho haambiwi ona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…