Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Pasco buana,bt pole kwa safari yenu ya matumaini ndani ya CCM kuishia Dodoma badala ya Ikulu ya Daresalam,so mtakaporudi Monduli pangeni safari nulyingine ya uhakika kupitia chama kingine
 
Nimepokea taarifa za uhakika kutoka kada mmoja mwandamizi wa Chadema, kuwa hatimaye Chadema kumekubali kuwa chama sikivu, kimekubali kubadilika na ndani ya saa 72, safari ya ukweli ya kuelekea ikulu, itatangazwa rasmi!.

Pasco
 
Mjadala huu ni very constructive.Niliona niwe msomaji zaidi ili niwe focused katika kujifunza,kweli wachangiaji wengi wametoa lecture ya kutosha kabisa!Bravo
Mkuu , asante, kama huu uvumi ulioeneo ni kweli, then safari ya Chedema kuchukua nchi kwa kishindo is for real, destination ni ikulu!.

Pasco
 
Cha kufanya wahusika kazeni nati sawa Sawa. Kuna kitu Pasco kaona... Hatujafika mwisho wa safari. Kumbukeni uzi uko hapa toka 2012
 
Pasco Mchambuzi Mzeemwanakijiji Nguruvi3
na wengine wote aiseee!!!
Nashindwa nisemeje kiukweli kupitia Uzi huu hasa, MUNGU ASIKIE KILIO HIKI Tafadhali!!

Maneno yamenikata ghafla baada ya kupitia kiasi hii thread!!!!
MUBARIKIWE TENA, NCHI HII IOKOKE NCHI HII IRUDI KWA WANANCHI, MUNGU daaaaah.....
 
Last edited by a moderator:
Article hii nimeisoma aisee

 
sio lazima lowasa awe rais aiseeee...na hawezi kuwa raisi sababu afai kuwa rais endeleeni kumpotosha tu.. mtavunja nguvu upinzani ulioanza kuimarika.. kwa uroho wa kura na wingi wa kufikirika wa wabunge walioshindwa kazi wakiwa ccm..kuna watu wengi mtawavunja nguvu mimi mmoja wao.. msimamo wangu uko wazi sina ushawishi chadema ila na ushawishi kwenye jamii inayonizunguka ntaimbia kama hili likitokea kuwa huu ni ulaghai wa kisiasa hakuna jina jingine..
 
Mkuu Maganga Mkweli, watu kama nyie ndio tunaowahitaji kuwaelimisha ili mkubali kubadilika!.

Kuna watu wa aina mbili, kuna ma conservatives ambao wao thinking yao ni static, hivyo wako stagnant na hawataki kubadilika wala hawataki mabadiliko yoyote, na hawa ndio wale ambao ama wanaichagua CCM despite all the odds, ama hawajiandikishi, na wakijiandikisha, hawapigi kura!.

Kuna liberals, hawa ni pro democracy, thinking yao ni dynamic, and hence they change with time!.

Just imagine, uko na mkeo kipenzi mnayependana sana, na mko safarini kwa usafiri wa meli, then kumbe kuna jamaa mnafahamiana mlisoma wote unakutana nae mmepoteana siku nyingi, mnaanza kupiga story, kukumbushana mliko toka na ku recap wewe ni nani na yeye ni nani, ndipo anakutajia yeye ni binga wa kuogolea, na sasa ameajiriwa kikosi cha zimamoto na uokoaji, na wewe unamueleza ni kibosile shirika fulani!, mnaendelea na kupiga story melini huku safari inaendelea!.

Huku yeye huyo jamaa hamjui mke wako!, katika mazungumzo yetu, mnakumbushana stori za ujana, kupiga mitungo na kuliana chabo na kuchapiana!, mara mke wako anakuja kwa mbali kuelekea sehemu ya kujisaidia, baada ya kukuona na huyo rafiki yako na yeye anashtuka ila anajikausha na kuwapita kimya!, mara huyo rafiki yako kwa kuzingatia mapito miliopita naye wakati wa ujana, anaamua kukupasulia kuwa leo ni siku ya furaha kubwa sana kwangu, huyu demu aliyetupita hapa, alikuwa demu wangu tangu zamani, mimi ndiye niliyekata utepe, ila siku hizi kaolewa ila kwa bahati mbaya muwe wake sio bingwa, hivyo huwa ananiletea angalau mara moja kila mwezi kwa ajili ya kumservice!, tena kiukweli ni mtamu balaa, kwa vile mimi sijaoa, kila akiniletea huwa ninamshawishi aachane na huyo mume wake aje mimi nimuoe, ananikatalia kuwa hawezi kuivunja ndoa yake kwa sababu tuu mumewe hamfikishi, ila anampenda sana na anaamini kuna siku atamfundisha jinshi ya kumfikisha, na muda huo ukifika, hizo servises zangu za kila mwezi zitakoma!.

Mara mke anatoka washroom na jamaa ndio anakuwa wa kwanza kumuita, darling, sweet heart, honey, come and meet my old school buddy!, ili wife asiunguze picha, anasema sorry utakuwa umenifananisha, mbona mimi sikujui!, jamaa akamtaja kwa jina kuwa sorry fulani, najua unazunga kwa sababu tunaiba tuu najua umeolewa!. Ndipo wife wako akakutambulisha kuwa huyu ndiye mume wangu!, na bila kuchelewa ulianza kupokea makonde mazito mazito toka kwa mwenye mali na wewe japo ni jitu la miraba minne ungejibu mapigo ungeweza kuua, ulikubali kupigwa huku umetulia tuu kama malipo halali kwa wizi wako wa kumega tunda la watu!. Mkaamuliwa mkaachanishwa, mume na mkewe wakaendelea kugombana kwa ahadi mke akifika nyumbani atamtambua!. Safari ikaendelea!.

Huku na huku, huku safari ikiendeleo, wewe unashikwa na tumbo la kuchafuka, unamuaga mkeo kwenda washrom, wakati ukiwa washroom, mara kunatokea tafrani ya bahari kuchafuka na meli kuanza kuzama, yule mkuu wa kikosi cha uokoaji aningia kazini, abiria wanavishwa maboya ya kuogelea na kutoswa baharini hadi wanakwishwa kumbe kuna mshenzi mmoja alifanya over booking ya abiria mmoja zaidi ya maboya yaliyopo, hata hivyo maboya yalitosha abiria wote wametupwa nje limebaki boya moja la mwisho la bingwa wa uokoaji ambaye anatakiwa kutoka ndani ya meli na kuiach meli sasa izame, ndipo captain anauliza abiria wote salama!.

Ndipo yule mke anapga yowe mume wangu alikwenda msalani hapa simuoni, ndipo bingwa wa uokoaji anakwenda kukfungulia huku amekubeba mzobe mzobe, akavaa boya lake na kusema lazima mtu mmoja afe maji kwa sababu maboya yamekisha, hivyo anakuacha kwenye meli inayozama ukipiga mayowe, yeye anavaa boya la mwisho kujiokoa!, huku mkeo akikushuhudia unakufa huku unajiona, yeke mke akamuomba yule bingwa wa ukoaji, bora afe yeye boya lake apewe mume wake kwa sababu angalau ana kipato, akifa mume familia itaisgia kuteseka!.

Bingwa wa uogeleaji, akaingiwa huruma akaamua kujitoa yeye maisha yake, kunusuru wewe, hivyo anarejea melini kukunyooshea a helping hand by that time uko kwenye maji ya shingo!, atafanya nini?. Utasusakuokolewa na mbaya wako kwa kuamua kuliko kudhalilika, akufungulie mkeo, akulie mkeo, akuokolee mkeo na sasa akuokoe na wewe?!, au bora ugome, ufe kishujaa, huku jamaa ajitwalie mkeo kama ameokota na kuiendelea kuishi raha mustarehe?!.

Hiki ndicho Chadema itakifanya ikiamua kumpokea Lowassa, haina maana Lowassa sasa ndio msafi, bali ndiye mtu pekee mwenye ufunguo wa geti la kuingilia ikulu!, Chadema kama ni kweli sasa iko serious na inataka kuingia ikulu, haina budi kumuangukia na kumnyenyekea mwenye ufunguo wa geti la ikulu, hata kama ufunguo huo umechafuka vipi!.

Bhari ndio uwanja wetu wa siasa, bingwa wa kuogolea ndie Lowassa, mkeo ndio Ikulu, na wewe ndio Chadema, kinapaswa kumkumbatia aliyekuwa adui, na kumtumia kujiokoa ili isizame tena!.

Hizi ndizo siasa!.

Jumapili njema!.

Pasco.






 
Mh! @ Pasco tangu jana nakuona ukifufua yaliyo pita hakika kuna habari kikubwa inakuja.....huu uzi ulikuwa constructive sana. Mungu ibariki Tanzania
 
Eti chadema kuchukua nchi endeleeni kuota.
Alafu unaposema ccm imechokwa tafadhali uwe unatumia data kuthibitisha hilo. Utafiti unaonesha chadema inashabikiwa sana katika hii miji michache. Sehemu nyingiii ni ccm bado.
Alafu chadema taasisi ya utatu Wa mbowe slaa na mtei hakiwezi kuwa chama Bali saccos.
Kwa kifupi chedema bado sana kuingia nyumba ya urithi
 
Shikamoo mzee mwenzangu Pasco. Nilianza zamani kusoma post zako kwa umakini, lakini kuanzia sasa nitazisoma sio kwa umakini tuu bali nitatumia na kurunzi pia kuona kuna nini back of the paper. Shukran.
 
Last edited by a moderator:
Safari rasmi inaanza kesho!, inaanzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kuchukua fomu!.
Pasco
 
Pasco unajua kuotea. Jaribu kucheza lotto unaweza kupata! Hahaha
 
While discussing about "safari ya matumaini/ mabadiliko/ kuingia Ikulu" we need to contemplate on the qualities of who would leads us there. Four qualities are paramount namely: BENEVOLENCE, RIGHTEOUSNESS, COURTESY, and WISDOM.
 
While discussing about "safari ya matumaini/ mabadiliko/ kuingia Ikulu" we need to contemplate on the qualities of who would leads us there. Four qualities are paramount namely: BENEVOLENCE, RIGHTEOUSNESS, COURTESY, and WISDOM.

Umeshachelewa, watu huwa wanahama mabondeni kabla mafuriko, its too late know.
 
While discussing about "safari ya matumaini/ mabadiliko/ kuingia Ikulu" we need to contemplate on the qualities of who would leads us there. Four qualities are paramount namely: BENEVOLENCE, RIGHTEOUSNESS, COURTESY, and WISDOM.
Mkuu Mwengeso, ukombozi wa pili wa Mtanzania, utapatikana kwa mtindo wa ukombozi wa wana Israel kutoka utumwani Misri, ndio jinsi ile ile Watanzania watakavyokombolewa toka utumwa wa CCM!.

Tena Mungu alivyo wa ajabu, alimpa Mussa kila uwezo wa kufanya ishara ili Firauni na watu wake waisikie Sauti ya Mungu, lakini hapo hapo, akaifanya mioyo yao iwe migumu, wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii ili aweze kujidhihirisha utukufu wake!, pale "Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Mwenye masikio na Asikie!.

Pasco
 

Mzee Pasco Shikamoo!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…