Mr Tyang
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 1,728
- 6,806
Kwenu Viongozi na wanabodi;
Bila kupoteza Muda naomba niende kwenye mada moja kwa moja; Leo nimekuwa nikijipa Muda wa kuchungulia kinachoendelea huku mitandaoni hasa JF na Twitter lakini Cha kushangaza nikuwa post nyingi nilizozipitia zimejaa hofu kubwa juu ya zoezi la kuwapata Wagombea urais wa JMT.
Hasa upande wa CHADEMA, baadhi ya Viongozi na wadau wa Chama hicho wamepost posts za hofu sana wakitahadhalisha Mgombea wao asienguliwe kwa Namna yeyote Ile, wengine wakaenda mbali zaidi kwa kusema kesho(25/08/2020) Dunia nzima itakuwa inatazama kinachoenda kutokea.
Je, hofu na wasiwasi huu uliotawala CDM Tatizo Ni Nini? Mgombea wa Chama hicho Hana vigezo kwa mjibu wa Sheria na taratibu za NEC?
Je, ni mbinu za kisiasa ili kuipa hofu NEC katika kufanya maamuzi yake sahihi kisheria na kitaratibu?.
Je kuanza kujiona umefeli angali matokeo hayajatoka Wala kusahihishwa nisawa?
Je, ikitokea NEC wamemupitisha huyo wanaezani hapiti Watakuja kuongea Nini tena au ndo wataivua nguo Tena NEC kuwa kusema bila wao NEC wasingempitisha?
Na je asipopitishwa kisheria Watachukua hatua gani?
Je, fomu za ugombea urais wamechukua Chama kimoja tu? Maana sioni Viongozi Wala wadau wa vyama vingine wakipost Wala kuwa na hofu juu ya mchakato wa kuwapata Wagombea urais wa JMT Hapo kesho isipokuwa CDM tu.
Ushauri Wangu; Naishauri NEC ifanye maamuzi yake yaliyo kwenye msitari wa Sheria na haki pasipo kuyumbishwa na mtu,Chama Wala kitu chochote kile. Pia Wagombea naomba Kama ukienguliwa kisheria Basi tafuta haki yako kisheria, siyo ukatwe kisheria halafu utafute haki yako kwa Nguvu Tena ya kuwatumia wenzio hizo siyo Akili za kiongozi aliye Bora.
Kila la heri kuelekea tukio kubwa la kuwapata Wagombea urais wa JMT 2020 pia tusisahau kuwa palipo na ushindani lazima Kuna kushindwa na kushinda.