Kuelekea AFL tujipange kuepuka aibu ndogo ndogo

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Ufunguzi wa michuano mikubwa zaidi barani Afrika inafanyika ijumaa hapa kwenye ardhi yetu. Kama kawaida yetu tunaweza kuchukulia rahisi sana fursa hii na tusijiandae kwenye mambo ya msingi kabisa. Hapa naweka dondoo chache za kuwa makini nazo;

1) Mashabiki wataokuwa uwanjani

Tuwe wastarabu na miundombinu ya uwanja. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake! Kutakuwa na wageni wengi ni aibu kukuta vyoo vina hali mbaya sababu ya kukosa ustaarabu.

2) Ushangiliaji wa wapenda soka

Tusianze uswahili wa kuzomea wachezaji wetu pale tumefungwa au anaingia mchezaji msiompenda. Kila mchezaji atayepewa nafasi tumpe hamasa sio vitimbwi na zomeazomea.

Pia si lazima tushangilie kama Mashabiki wa EPL, Tunaweza kushangilia kwa styles zetu na kucheza kivyetu kama singeli n.k.

3) Vyombo vya usalama

Hapa sasa ndio muhimu zaidi. Wapewe seminar namna ya ku handle Mashabiki sio kupiga virungu huku International media zina rekodi itakuwa aibu.

Askari wetu wavae uniform za kupendeza wawe smart na zana zao. Askari waelekezwe namna ya ku behave dunia isitushangae.

4) Utaratibu wa kuingia uwanjani

Uwekwe utaratibu mzuri wa kistaarabu na mageti yafunguliwe mapema. Ni aibu pia watu wenye tiketi kushindwa kuingia. Kuwe na udhibiti mkali wa tiketi feki.

5) Ulinzi nje ya uwanja

Vyombo vya usalama viimarishe ulinzi eneo lote kuzunguka uwanja. Hizi siku vibaka hawana rangi, unaweza kupigwa roba na mtu kavaa reflector kama mmoja ya wahusika wa ulinzi shirikishi.

Mwisho, hili ni tukio kubwa na la kihistoria, tuepuke aibu ndogo ndogo kwa kukosa tu ustaarabu. Tutatia aibu zaidi ikitokea hilafu za umeme kama kawaida yetu. Tuipe heshima taifa letu alafu Simba SC wamalize na ushindi kunogesha zaidi.

Kila lakheri Mnyama, Lunyasi!
 
Namba 2 ni muhimu kujizuia, Kuna kipindi Kila mtu anaona mchezaji hayuko mchezoni ama analeta madhara kwenye timu au anakosa nafasi za wazi lakini kocha bado kocha hamfanyii mabadiliko hapo hata Mimi huwa nazomea toa Hilo.
 
Vema , bila shaka wahusika watafanyia kazi
 
Ikiwezekana hiyo namba 1 basi yote yatawezekana,namba 1 ndio msingi wa yote hayo "Ustaarabu'' Discipline and attitude,

Discipline is the bridge between goals and accomplishment.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…