MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Ufunguzi wa michuano mikubwa zaidi barani Afrika inafanyika ijumaa hapa kwenye ardhi yetu. Kama kawaida yetu tunaweza kuchukulia rahisi sana fursa hii na tusijiandae kwenye mambo ya msingi kabisa. Hapa naweka dondoo chache za kuwa makini nazo
1) Mashabiki wataokuwa uwanjani
Tuwe wastarabu na miundombinu ya uwanja. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake! Kutakuwa na wageni wengi ni aibu kukuta vyoo vina hali mbaya sababu ya kukosa ustaarabu.
2) Ushangiliaji wa wapenda soka
Tusianze uswahili wa kuzomea wachezaji wetu pale tumefungwa au anaingia mchezaji msiompenda. Kila mchezaji atayepewa nafasi tumpe hamasa sio vitimbwi na zomeazomea.
Pia si lazima tushangilie kama Mashabiki wa EPL, Tunaweza kushangilia kwa styles zetu na kucheza kivyetu kama singeli n.k
3) Vyombo vya usalama
Hapa sasa ndio muhimu zaidi. Wapewe seminar namna ya ku handle Mashabiki sio kupiga virungu huku International media zina rekodi itakuwa aibu.
Askari wetu wavae uniform za kupendeza wawe smart na zana zao. Askari waelekezwe namna ya ku behave dunia isitushangae.
4) Utaratibu wa kuingia uwanjani
Uwekwe utaratibu mzuri wa kistaarabu na mageti yafunguliwe mapema. Ni aibu pia watu wenye tiketi kushindwa kuingia. Kuwe na udhibiti mkali wa tiketi feki.
5) Ulinzi nje ya uwanja
Vyombo vya usalama viimarishe ulinzi eneo lote kuzunguka uwanja. Hizi siku vibaka hawana rangi, unaweza kupigwa roba na mtu kavaa reflector kama mmoja ya wahusika wa ulinzi shirikishi.
Mwisho, hili ni tukio kubwa na la kihistoria, tuepuke aibu ndogo ndogo kwa kukosa tu ustaarabu. Tutatia aibu zaidi ikitokea hilafu za umeme kama kawaida yetu. Tuipe heshima taifa letu alafu Simba SC wamalize na ushindi kunogesha zaidi.
Kila lakheri Mnyama, Lunyasi!