Kuelekea Derby: Yanga yalaumiwa na Bodi ya Ligi

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imesema haipendezwi na tabia ya timu mgeni kwenye Mchezo wa Kariakoo Derby kutoifanyia promo mechi ya derby na kuachia jukumu hilo kwa timu mwenyeji pekee.

Akizungumza na kituo cha Clouds fm radio msemaji wa bodi ya ligi, Karim Boimanda amesema mchezo huo si tu kwa ajili ya mapato ni Mchezo mkubwa Nchini na Afrika mashabiki hivyo vilabu vyote viwili (2) vinapaswa kuipromoti mechi hiyo.

"Hii inatokana na kanuni ya kuwa timu mwenyeji ndio atapata mapato yote ndio maana timu mgeni hafanyi promo, bodi ya ligi hatufurahishwi na jambo hilo tutalifanyia kazi suala hilo. Mechi hii sio tu kwa ajili ya mapato ni mechi ya hadhi ya Nchi" amesema hayo Karim Boimanda.
 
Boimanda amefikiri kwa kutumia Tumbo......kwani wao Bodi ya Ligi wanazuiwa kuifanyia promo mechi ya Derby...

Watoe fungu la promo kwa Klabu husika, sio kusubiria mapato tu....

Promo ni pesa....

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Boimanda amefikiri kwa kutumia Tumbo......kwani wao Bodi ya Ligi wanazuiwa kuifanyia promo mechi ya Derby...

Watoe fungu la promo kwa Klabu husika, sio kusubiria mapato tu....

Promo ni pesa....

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Kashaona maokoto yatapungua, na Ahmed Ally kuelekea hii match kapoa mno naona kashajua kipigo kinawahusu.
 
Boimanda hapa kapuyanga sana kimsingi Simba ndio waanzilishi wa huu mchezo wa kugoma kuitangaza mechi ya watani pale yanga anapokuwa mwenyeji

Na mbona tamasha la Simba day lilijaa Sasa wanashindwa Nini kuijaza trh 5 hadi waanze kuisakama yanga au wanataka kupiga fine
 
Hata Azam nao wana matangazo ya kiboya yasiyohamasisha hata watu kununua visimbuzi vyao kama ambavyo derby nyingine huko nyuma walivyokua na ubunifu kwenye matangazo yao.

Uwanja utapwaya sana hiyo siku.
 
Akizungumza na kituo cha Clouds fm radio msemaji wa bodi ya ligi, Karim Boimanda amesema mchezo huo si tu kwa ajili ya mapato ni Mchezo mkubwa Nchini na Afrika mashabiki hivyo vilabu vyote viwili (2) vinapaswa kuipromoti mechi hiyo.

Huyo jamaa alikuwa katoka kunusishwa harufu ya bangi ama?
 


Uzuri mumefahamu kama mna sheria mbovu inayopendelea timu mwenyeji kuchukua mapato yote huku mgeni akibaki mikono mitupu wakati TFF na Bodi ya ligi wanapata mgao wa pesa nyingi za kunyonga. Alafu yote hayo mnaishia kulaumu timu mgeni kutofanya promo tena kwa gharama zake sio zenu nyie wafaidika. Jambo hili sio zuri, badilisheni hii sheria ili kila kitu ifanye promotion wakiwa wanafahamu kuwa kwenye mgao watapata chochote.

 
Shida imeanzia hapa
 
Hawa Wasemaji wasio na mipaka na Bodi kuwakalia kimya ndo chanzo cha hili tatizo.
Kuna Mechi naikumbuka vizuri timu moja iliwatangazia mashabiki wake kwenda Kwa wingi uwanjani wakiwa timu mgeni lakini msemaji wa timu mwenyeji akaibuka na kusema hii siyo Mechi yao na hakukemewa. Nilijiuliza labda kuna kanuni huko TFF inazuia timu mgeni kupromote Mechi kumbe ndo nasikia Hakuna kanuni Kama hiyo.
 
Kwa wenzetu mwenyeji huwa anatoa idadi ya ticket, say 5000, kwa mashaibiki wa timu ngeni zinazobaki ni za wenyeji. Hapa ikoje? The last time nilingia uwanja wa taifa ilikuwa 1981 na sikupenda kabisa mipango yao. Ilkuwa mechi ya Yanga vs Simba. Naona bado ubabaishaji upo zaidi ya miaka 40 after. Pathetic.
 
How old are you now?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…