Kuelekea Dira Mpya ya Maendeleo 2050: Natamani Tanzania iwe namba 4 kwa uchumi Afrika na kuzipita Algeria, Morocco, Angola, Kenya na Ivory Coast

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Tanzania imeandaa Dira Mpya ya Maendeleo ya 2050 ambapo utekelezaji wake utaanza rasmi mwaka 2025/26 baada ya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge kabla ya Rais kuidhinisha rasmi.

Kwa Sasa Serikali imezindua rasimu na ambapo zoezi la maboresho linaendelea ikiwemo kutoa maoni.

Sasa Kwa wapanga mipango pamoja na kuweka malengo ya kuwa na GDP ya $ 700bln na per Capita income ya $4700 by 2050 napendekeza pia tuweke kigezo Cha kiushindani na Nchi zingine Ili tuwe tunajipima na wengine.

Tunapoanza utekelezaji wa Hiyo Dira Natamani inapofika mwaka huo au kabla ya mwaka huo basi Tanzania iwe ni Kati ya Nchi 5 Zenye Uchumi mkubwa Barani Afrika ambapo tunatakiwa kutoka nafasi ya 10 tuliyoko Sasa Hadi kufikia nafasi ya 4 na kama.tukishindwa basi tuwe nafasi ya 5.

Tanzania tuna sababu na vigezo vyote vya kufikia nafasi ya 4 Kwa kuanzia na Rasilimali asili zilizopo.

Nafahamu Kila Nchi Ina Mali asili lakini Kwa Tanzania tutakuwa na advantage ya idadi kubwa ya watu.

Kwa Sasa Tanzania ni namba 5 kwa Wingi wa watu hapa Afrika na bila shaka tunaendelea kuwa namba 5 miaka Mingi ijayoa Sasa inatakiwa tutumie Wingi wetu kuwa fursa ya soko na Uchumi Ili tukuze Uchumi wa Nchi yetu.

Kama tumeweza kuingia top 10 Kwa nini tushindwe kuwa namba 4?



Hivyo basi by 2050 ni matumaini yangu kwamba Msimamo wa Ligi ya Uchumi Afrika Mwaka 2050 utakuwa kama ifuatavyo.,

1.Nigeria
2.Egypt
3.Ethiopia
4.Tanzania
5.Algeria
6.South Africa
7.DR Congo
8.Morocco
9.Angola
10..Kenya
11.Ivory Coast
12.Uganda.
 
GDP per capita ndio jambo muhimu zaidi, uchumi mkubwa haukusaidii chochote kama GDP per capita yako ndogo.

Nigeria, Ethiopia, India, Pakistan na Bangladesh ni mataifa yenye GDP kubwa ila raia wake wengi wanaishi maisha duni sana.
 
Iwe Namba one 🐼

Prof Mkumbo na Dr Mwigullu PhD mtuvushe 🌹
Namba baadae sana ,unaweza ivuka Algeria,South Africa ila sio Nigeria, Egypt na Ethiopia,hao Wana watu wengi.

Nchi zote Zenye watu wengi Duniani ndio zinaongoza Kiuchumi,hata Germany anaongoza Kwa Wingi wa watu Ulaya.
 
Kuna Nchi ngumu sana Kuzipita, Kama Algeria soon Watakuwa na Uchumi mkubwa Africa wana Miradi ambayo haijapata Tokea Africa, na wanakua kwa kasi sana.

Ila Nchi kama Kenya it's doable, Soon tunawapita.
Uko sahihi nimeifuatilia Algeria nimeona wako na mamiradi makubwa na wanatumia vizuri utajiri wao wa gesi.

Hata hivyo kama tutaweka sera za kukuza kipato Cha mtu mmja mmja Ili kuongeza purchasing power tunaweza walau kuja kuwafikia.

Mwisho Nchi nyingine ambayo inaweza kuwa tishio Kwa Tanzania ni DR Congo.
 
Kwamba South Africa itakuwa nje ya top 10?! Nyie ndio mnasababisha bangi inakatazwa.
 
Kuna Nchi ngumu sana Kuzipita, Kama Algeria soon Watakuwa na Uchumi mkubwa Africa wana Miradi ambayo haijapata Tokea Africa, na wanakua kwa kasi sana.

Ila Nchi kama Kenya it's doable, Soon tunawapita.
Hata Kenya hatuwapiti soon,
 
Miaka 10 sio mapema na hata hivo hizo ndoto zinaweza zisitimie.
Nakuhakikishia zitatimia ingawa zimechelewa,projection ya awali ilikuwa 2028 lakini sioni huo uwezekano.

Ila kati ya 2030-2034 hapa lazima tuwakalishe Ili tuanze kuwatafutia hao wengine.
 
Hata Kenya hatuwapiti soon,
Isingekuwa Magu tungekuwa tunawakamata tena hawa.

Mkapa na Kikwete walikua na Stable Economic growth, Mfano Kipindi Cha Kikwete Economic Growth mwaka Mmoja tu kati ya 10 ndio ilikua asilimia 4.5 ila miaka yote ni Asilimia 6 ama 7, Kidunia tulikuwa one of the best, roughly Estimation tungekuwa na Same Growth kama ya Kipindi cha Kikwete sasa hivi Gdp per capita yetu ingekua $1700-1800 na Kenya $1900. Ila sasa hivi tupo $1200.
 
Pamoja na kwamba jiwe hakuwa na sera nzuri za kukuza uchumi ila miaka miwili ya COVID iliharibu chumi za mataifa yote ya dunia. Ni jiwe pia aliyehakikisha kunakuwa upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme na miondombinu ya reli vitu ambavyo ni muhimu sana katika kukuza uchumi kwa malengo ya muda mrefu.
 
Huyo Magu ndio mtoe, uchumi ulidumaa sana awamu yake na ndio Kenya iliweka Gap kubwa.

Uchumi ni namba sio hisia ,awamu ya 6 ndio inaziba Gap la awamu ya 5.
 
Nishati ipi ya umeme ilipatikana awamu ya Jiwe Mzee? Kuna chanzo chochote kipya kilikuwa kinazalisha umeme?

In fact uchumi ulikuwa stagnant sana miaka 5 ya Jiwe na ndipo Wakenya walipanua Gap zaidi ambalo lilikuwa limeounguzwa zaidi na JK.

Awamu ya Mkapa Uchumi wa Tanzania na Kenya ulikuwa at par lakini tukaja kuachwa miaka 5 ya mwisho ya Mkapa.
 
GDP ya Tanzania mwaka 2016 ilikuwa bilioni $49, mwaka 2021 ilikuwa bilioni $70
 
Boss Kikwete Katuongoza kwenye Great Economy Recession 2007-2009 na hatukudorora ukuaji. Hapo uchumi ulishuka vibaya mno Kidunia kuliko Covid.

I doubt reli is that important mkuu kwenye Uchumi wetu kushinda Barabara zinazo connect nchi na mikoa, so far ni luxury tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…