Kuelekea dirisha Dogo la usajili: Tetesi za usajili Simba S.C

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
1. Kuhusu zile tetesi za mshambuliaji bora kabisa kwa sasa katika KPL, Raphael Kiongera kurejea Msimbazi...

Raphael Kiongera mwenyewe kanena haya... "Sasa ninajiandaa kurudi Simba nikapiganie nafasi yangu. Najua wamefanya mabadiliko ya hapa na pale katika kikosi, lakini nina imani nitapigania nafasi yangu ili niendeleze fomu yangu hapo Msimbazi."
NB: Fomu anayoizungumzia ni kutupia goli 11 katika mechi 17 za KPL.. pia alikua mchezaji bora wa mwezi wa 8.
Source: Kiongera anakuja kuwanyoosha

2. Kuhusu tetesi za mshambuliaji bora kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini Burundi [achana na amis], kutua Msimbazi.. Laudit Mavugo...

Simba haitaki mchezo kabisa katika hili suala kwani imetenga kiasi cha dau la dola 50,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 100 ili iweze kumnasa.
Chanzo chetu toka jikoni kinatujuza.... "Kama asipotufanyia uhuni, basi tutamsajili lakini akileta tamaa ya fedha tutamwachia aende zake, ila kusema kweli tunamuhitaji na tayari tumeshaanza naye mazungumzo.

Source: SIMBA YARUDI TENA, YATENGA MAMILIONI MENGINE IMSAJILI MRUNDI MAVUGO - SALEH JEMBE

3. Kuhusu kumsajili Didier Kavumbagu...

Kocha Mkuu wa Simba S.C ambae anamiliki leseni ya juu kabisa ya ufundishaji soka toka UEFA.. Dylan Kerr, kanena haya.... "Huyu jamaa anaonekana anajua sana kufunga, amekuwa na kiwango kinachofanana kwa miaka yote, kama anataka kuja Simba ni poa tu, nitajadili na viongozi tuone cha kufanya."

Source: Simba yachukua beki Tanga, Kavumbagu freshi tu

4. Unamkumbuka Erisa Ssekisambu?
Huyu ni mshambuliaji hatari sana wa Vipers na timu ya Taifa ya Uganda 'Cranes'.. Huyu jamaa ndo alitupia goli lilioifanya Taifa Stars ishindwe kushuriki michuano ya CHAN mwakani...
Kuna tetesi kua anataka kutua Msimbazi..

Erisa Ssekisambu kanena haya... ''Simba bado hawajanifuata, kama wana mpango huo mimi sina tatizo ila wao ni kufuata taratibu kwa kumalizana na viongozi wangu kwani nina mkataba wa miaka mitatu... wakileta pesa hakuna shida''

NB: Kama aliweza kuifanya beki ya Taifa Stars [nadir + yondan + shomari] ilale na viatu.. naamini atafanya makubwa sana.
Source: ERISSA: SIMBA WALETE PESA NIJE | BOIPLUS Blogspot

5. Baada ya kuonekana kuna tatizo pindi aumiapo beki wa kati.. Kuna tetesi kua Mnyama kaingia sokoni kutafuta Beki kisiki wa kuimalisha Great Wall of China...

Evance Aveva kalizungumzia hilo..
"Tunatarajia kuipata ripoti ya kocha kesho, lakini katika mazungumzo ya awali ametuambia kuhusu mahitaji ya beki wa kati na tumekwishaanza kulifanyia kazi."
Kuonesha ni kwa jinsi gani uongozi ulivyo serious.. Kambi ya African Sports imevamiwa, lengo ni kumnasa beki kisiki.. Novatus Lufungo. Uongozi wa African Sports umecharuka na kutoa tamko hili... ?Tumesikia taarifa hizo kupitia kwa mtu ambaye Simba wanamtumia, lakini- wafuate utaratibu wa usajili, Nova ana mkataba, hawapaswi kuanzia pembeni."

Source: Simba yachukua beki Tanga, Kavumbagu freshi tu

6. Lastly on Kevin Ndayisenga...

The marauding forward said his earlier attempt to join the Tanzania Mainland heavyweights was futile following a disagreement during negotiations in the eleventh minute.
"It is a big club and nobody in this region can decline an opportunity to play for them. I am ready to sign the contract anytime."
Source: Burundian ready to ink for Simba SC


Nachoamini.. Dirisha Dogo litakapokua linafungwa.. 95℅ of this romours will be reality.

Simba Sports Club.. Nguvu Moja
 
...akipatikana mavugo au kavumbagu na beki mmoja wa kati wa maana kwangu wanatosha..
 
...akipatikana mavugo au kavumbagu na beki mmoja wa kati wa maana kwangu wanatosha..

Hicho ndicho kinachofanyika.. Kwa sasa tuna midfield bora kabisa katika VPL.. Naamini kabla ya kuanza mzunguko wa 2 hapo 12/12/2015 [dhidi ya Azam].. Tutakua tushapata majembe ya uhakika kwa ajili ya kuongeza nguvu.
 
Naona lile tatizo sugu la pesa pale simba limeishapata ufumbuzi
 
Kutamani jambo moja. Kuwa na uwezo wa kufanikisha jambo lingine.
 
Okwi vipi ??harudi??

Mkuu kwa soka la kiwango cha juu jabisa Okwi analosakata kwa sasa.. Ni ngumu sana kuja kucheza Africa.. Meib baada ya miaka mingi ijayo.
Kuna tetesi kua vigogo wa EPL wanapigania saini yake na kuna uwezekano akatua uingereza Jan. 2016.. Hebu tuwe na subira.
 
Huyo Kiongera akitua Simba anarogwa tena, safari hii hatarudi tena
 
Huyo Kiongera akitua Simba anarogwa tena, safari hii hatarudi tena

Mkuu wachezaji wanaoongoza safu ya ushambuliaji ya sasa ni tofauti na wa kipindi kile.. Na kama alikua anapigwa misumari.. Naamini wabaya wake wote washaondoka.. Hivyo akitua ashindwe mwenyewe.

Na nilichokipenda zaidi toka kwake ni hii kauli yake... "Sasa ninajiandaa kurudi Simba nikapiganie nafasi yangu. Najua wamefanya mabadiliko ya hapa na pale katika kikosi, lakini nina imani nitapigania nafasi yangu ili niendeleze fomu yangu hapo Msimbazi."
 
...akipatikana mavugo au kavumbagu na beki mmoja wa kati wa maana kwangu wanatosha..

Mkuu, beki wa kati kashapatikana, ni yule "Beki Kisiki" Novatus Lufunga.. Though bado tunahitaji mshambuliaji.. ila ujio.. wa Danny Lyanga na Kiongera.. utaongeza healthy competitions pale mbele.


Kutamani jambo moja. Kuwa na uwezo wa kufanikisha jambo lingine.

Mnyama kashaanza kuchanua makucha yake.. Novatus Lufunga atua rasmi.
 


Hahaha. Hata hivyo wachezaji hata wawe wazuri kiasi gani lazima wakae pamoja kwa muda wa kutosha. Pili, kocha pia awe na timu muda wa kutosha na asiingiliwe kwenye kazi yake na akina Hans Pope kumpangia timu. Wamwachie afanye usajili yeye.

Nashukuru Yanga wameyaona hayo kwa sasa na matunda tunayaona!
 

Atatua Uingereza ipi,ile ya Goms?
 
Uzuri wa VPL ni kwamba bado Simba ina nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa game tulizocheza nyingi tumebalance,home and away.
Karibu Lufungo,Kiongera na Lyanga(dan)-ITC iko poa.
 

Huyo Lufunga katokea timu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…