Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Kuna timu zina wachezaji wenye majina makubwa lakini sio ndio garantii ya kufanya vyema hasa linapokuja suala la Tournament kubwa kama hii ya Euro 2016 ambayo itafanyika Ufaransa kwanzia 10 June mpaka 10 July na kushirikisha jumla ya timu 24.

Leo nataka tujadiliane timu ambazo zitafika mbali yani kwanzia nusu fainali mpaka fainali kutokana na uhodari wa vikosi vyao, kujituma kwa wachezaji pamoja na makundi waliyopo.


Mimi nazipa nafasi timu hizi nne kufika mbali zaidi.
1.Ufaransa
Licha ya kuwa wenyeji tu bali pia wana kikosi cha dhahabu kama vile Pogba, Martial, Griezmann, Laporte, Coman, Benzema na wengineo wengi.

2.Ubelgiji
Kikosi kingine ninachokipa nafasi kwa kuwa timu yenye wachezaji wenye muunganiko mzuri.

3.Ujerumani
Never underestimate the Germans.
Kitu pekee ninachowapa nafasi hawa jamaa ni uwezo wao wa kuwa na wachezaji wenye kujituma sana hasa linapokuja suala la kuvaa jezi ya timu ya taifa. Wana wachezaji ambao huwa hawavumi sana katika klabu zao ila wanapafomu vizuri timu ya taifa. Rejea kuhusu mkongwe aliyestafu Miroslav klose.

4.Croatia
Watu wengi hawazungumzii kuhusu Croatia ila balaa lake ni moto wa kuotea mbali kuna mafundi wa kutosha wasioimbwa ulaya kama akina Kovacic, Modric, Rakitic na wengineo.

Karibu utuambie na wewe timu unazozipa nafasi kufanya vyema kwenye Euro 2016 pale Ufaransa.

========================================================================================================

Ratiba kamili na muda hii hapa chini

 
Mimi timu iliyo na wachezaji wa Barcelona ndiyo itakayotwaa ndoo na jambo la kujivunia Barcelona haina mchezaji Muingereza wala Mreno maana hz timu mbili ni washiriki haswahaswa huyo vuvuzela England aliyejaza wachezaj kibao wa man u ambao sifa za media 90% uwezo wa huyo anayepewa sifa 10%
 
Hapo kwenye Croatia muongeze dogo anayecheza Sporting Gijon anaitwa Hallen Hallilovic huyo mtoto ni fundi haswaaa wala habahatishi kama Rashford Martial au Iwob hata jana kawasumbua sana Israel had alipotoka ndio wakaanza kupumua
USINIULIZE CLUB YAKE WAKAT NISHAKWAMBIA YUPO SPORTING GIJON
 
Germany . france, spain, belgium
 
France balaa Ngolo kante, blessed matuid, grizman, benzema, martial, lloris, pogba, payet(westham) ,.....malizieni jmn sio euro tu world cup 2018 moto watauwasha
 

Naona una chuki na Man U. Kutoka Man U ni Chris smalling tu. Sidhani hata kama carrick ameitwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…