Uchaguzi 2020 Kuelekea Ikulu ya Tanzania 2020 yupo wa kushindana na Magufuli

Uchaguzi 2020 Kuelekea Ikulu ya Tanzania 2020 yupo wa kushindana na Magufuli

Dr Pesambili

Member
Joined
Apr 15, 2018
Posts
9
Reaction score
77
Ni nani hasa ambaye anaweza kunipa ushahidi wa dhati ambao hata nafsi yake inakiri kuwa ni wa kweli, Kuelekea IKulu ya Tanzania 2020 yupo wa kushindana na Magufuli? Hakika kama yupo anaweza kunisaidia nami kujua.

Huyu wa kushindana nae atakuja na ajenda gani? Hawa wapinzani hivi ni kipi hasa ambacho wameweza kutueleza hadi sasa ambacho kweli kinahalalisha uwepo wao katika kinyang’anyiro hiki, achilia mbali kuchaguliwa kutuongoza? Ndio, ni kipi hicho ambacho nyie mmekiona mnisaidie .

IMG_20200712_083708.jpg
 
Kama polisi wenu, mahakama yenu,msajili wenu lakini upinzania wakifanya mkutano hata wa ndani mavi yanawabana.

Yapo mambo mengi ya kumkosoa Magu ndio maana akisikia upinzani wanafanya mkutano, wanatuma polisi.

Moja ya point

Kuna viongozi waliwahi kukaririwa wakisema kama hamchangui chama fulani hatuleti maendeleo. Najiuliza watu hawa wanalipa kodi bila ubaguzi, ila kwenye maendeleo tunawabagua.
 
Dr. Pesambili. Hapa nimejiuliza hii “Dr.” ni tabibu wa binadamu au ni wa falsafa? Ikiwa ni jambo la pili - ndio hasa sababu kwanini taifa hili halitasonga mbele!!

Tumekwama kwa sababu watu kama ninyi hamna fikra, mna macho. Daktari wa falsafa anapaswa kuona kwa fikra!!

Ujinga, maradhi na umasikini ni maadui zetu wa kuu. Wanaweza kuonekana wana viwango sawa lakini ujinga ni mkubwa sana!! Wewe utakuwa mwanaCCM mwaminifu, ni jambo zuri.

Kinachonitatiza wewe badala ya kushindanisha upinzani na CCM wakati hawako katika mizania sawa. CCM na fikra zake vimekuwa madarakani toka 1961. Upinzani haukuwahi kuwa madarakani kabisa.

Lakini hapa unavishindanisha!! Unaona wako na level playing ground! Wote wana nguvu sawa. Bila shaka vitu unavyoona kama madege, reli, bwawa, elimu bure unaviona kama ni mambo makubwa.

Ni kweli ni makubwa. Lakini umejiuliza zaidi kuhusu ubora, ufanisi, uendelevu wake?? Hayo ndio mambo ya akili - sio macho!! Ili kufahamu mambo hayo uhuru wa watu kutoa maoni upewe nafasi.

Watu wautumie vizuri na wasikilizwe na wanaoutumia vibaya waadhibiwe, sheria zipo!!! Ubaya wa sasa, hakuna mtu anayetoa mawazo yake kwa uhuru akabaki salama na kama ni ushindi huo unauzungumzia kwa mantiki hiyo - ni kweli hakuna wa kushindana na Magufuli. Walio wengi wanashindana nae kifikra na hawana uwanja sawa.

Iko siku nawe utashindana nae kifikra, kwa sasa hushindani nae - macho yako ndio yanaongoza akili zako. Siku akili ikianza kukuongoza, utafikiri tofauti hasa kuhusu ubora wa elimu, ufanisi wa ndege, swala la uwazi, dhuluma kwa mawazo huru nk.
 
We Pesambili ya mtwara au wapi, ulitaka wapinzani wajinadi kwa kujenga barabara?
 
Huu ujinga utaisha,walikuwepo kina Saddam Hussein na wengineo waliokuwa wanapata ushindi wa asilimia kama hizo ila leo imabaki historia tu.

Na historia hio ni pamoja na masanamu yao kuvunjwa na kupondwapondwa.
Ingekua vema ungemjibu kwa hoja alizouliza
 
Jamaa ana roho mbaya kama sura yake kwenye hiyo picha
 
Back
Top Bottom