Dr. Pesambili. Hapa nimejiuliza hii “Dr.” ni tabibu wa binadamu au ni wa falsafa? Ikiwa ni jambo la pili - ndio hasa sababu kwanini taifa hili halitasonga mbele!!
Tumekwama kwa sababu watu kama ninyi hamna fikra, mna macho. Daktari wa falsafa anapaswa kuona kwa fikra!!
Ujinga, maradhi na umasikini ni maadui zetu wa kuu. Wanaweza kuonekana wana viwango sawa lakini ujinga ni mkubwa sana!! Wewe utakuwa mwanaCCM mwaminifu, ni jambo zuri.
Kinachonitatiza wewe badala ya kushindanisha upinzani na CCM wakati hawako katika mizania sawa. CCM na fikra zake vimekuwa madarakani toka 1961. Upinzani haukuwahi kuwa madarakani kabisa.
Lakini hapa unavishindanisha!! Unaona wako na level playing ground! Wote wana nguvu sawa. Bila shaka vitu unavyoona kama madege, reli, bwawa, elimu bure unaviona kama ni mambo makubwa.
Ni kweli ni makubwa. Lakini umejiuliza zaidi kuhusu ubora, ufanisi, uendelevu wake?? Hayo ndio mambo ya akili - sio macho!! Ili kufahamu mambo hayo uhuru wa watu kutoa maoni upewe nafasi.
Watu wautumie vizuri na wasikilizwe na wanaoutumia vibaya waadhibiwe, sheria zipo!!! Ubaya wa sasa, hakuna mtu anayetoa mawazo yake kwa uhuru akabaki salama na kama ni ushindi huo unauzungumzia kwa mantiki hiyo - ni kweli hakuna wa kushindana na Magufuli. Walio wengi wanashindana nae kifikra na hawana uwanja sawa.
Iko siku nawe utashindana nae kifikra, kwa sasa hushindani nae - macho yako ndio yanaongoza akili zako. Siku akili ikianza kukuongoza, utafikiri tofauti hasa kuhusu ubora wa elimu, ufanisi wa ndege, swala la uwazi, dhuluma kwa mawazo huru nk.