Lord Delamere in Kenya
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,988
- 8,021
Zingatia:Kabla sijaenda mbali zingatia hili-katika mara zote walizokutana Simba SC haijawahi kuifunga Nkana au kutoa droo pale Kitwe,Zambia.Halikadhalika NKANA HAIJAWAHI KUIFUNGA au KUTOA DROO NA SIMBA HAPA NYUMBANI,TANZANIA.Nkana amekuwa akisonga mbele kutokana na kufunga magoli mengi akiwa kwenye "machinjio" yake ya Kitwe.
Mwaka 1994 nilikuwepo Uwanja wa Taifa wa zamani,siku hizi mnauita Uwanja wa Uhuru,kwenye mtanange wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba vs Nkana Red Devils.Enzi hizo Nkana ilikuwa timu hatari kule Zambia sambamba na Mufulira Wonderers,hawa akina Zanako sijui Zesco tumeanza kuwasikia juzi juzi tu.
Ikumbukwe,Simba hii ya mwaka 1994 ilikuwa imeingia kwenye Robo Fainali ya mashindano hayo ya CAF Champions League.Na mwaka mmoja nyuma,1993,ilikuwa imecheza Fainali ya kombe la Shirikisho CAF na kufungwa na Stella Abdjan ya Ivory Coast.Simba ya miaka hiyo ilikuwa moooto wa kuotea mbali ikiwa na wachezaji mahiri kama Mohammed Mwameja,Kasongo Athumani,Deo Mkuki,George Masatu,akina Malota Soma "Ball Juggler" ,Edward 'Edo' Chumila,n.k.
Simba hiyo haikucheza na Nkana FC ya kitoto,bali ilikuwa Nkana 🔥 vile vile.Ilikuwa na wachezaji nyota kama Joel Kangwa Bwalya,Mathias Mulenga,Harrison Chongo,Mordon Malitoli na mdogo wake Kenneth Malitoli (captain).Nyota hao wa Nkana Red Devils walikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Zambia,kilichocheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria mwaka huo wa 1994,na Super Eagles kubeba kombe kwa ushindi wa magoli Nigeria 2 - 1 Zambia,magoli yote mawili ya Nigeria yakifungwa na mchezaji hatari EMMANUEL AMUNIKE (huyu huyu tunayemdharau leo hapa Bongo),huku lile la Zambia likifungwa na beki ELIJAH LITANA.
Hebu tazama vikosi vikali vilivyocheza kwenye Fainali ya Kombe la Mataifa ya Africa 1994,na uone wachezaji wa nyota was Nkana (in bold) walivyopambana kiume na nyota wa Nigeria.
Nigeria: Peter Rufai,Uche Okwechukwu,Uche Okafor,Ben Iroha,Augustine Eguavoen,Emmanuel Amunike, Austin 'Jay Jay' Okocha,Sunday Oliseh (captain wa ukweli)Finidi George,Daniel Amokachi na Rashid Yekini.Benchi walikuwepo Samson Siasia,Nduka Ugbade,kijana Mutiu Adepodju,n.k
Mwaka huo Rashid Yekini(RIP) ndo alikuwa mchezaji bora wa AfCON.Atakumbukwa zaidi kwa yale ma-acrobatics yake ("tik - tak") kama ya Ibrahim 'Cadabra' Ajibu.Maana Yekini alikuwa anayapiga sana hadi kero.
Zambia:James Phiri,Harrison Chongo,Elijah Litana,Mordon Malitoli,Aggrey Chiyangi,Mathias Mulenga,Evans Sakala,Kenneth Malitoli,Joel Kangwa Bwalya,Zeddy Saileti,na mtaamu mwenyewe Kalusha Bwalya.Huku benchi akiwepo Linos Makwaza,Johnson Bwalya,n.k (na hawa akina Bwalya we wasikie tu!..Naamini mmoja mlimwona juzi kule Kitwe,na Jumapili atakuwepo).
Simba iliingia uwanjani siku hiyo ikiwa na lengo la kufika mbali na kufuta mashabiki wao machozi,kutokana na kadhia ya kufungwa kwenye fainali ya kombe la CAF. "Washkaji" wengi wa kijiwe chetu cha Squad pale mitaa ya Wailes,Temeke mwisho na Kitomondo tulikuwepo kuwatazama Masela wenzetu akina George Masatu,Ramadhan Lenny (RIP),Edward Chumila,na George Lucas "Gazza" wakiwapiga 2 - 1 Nkana FC.
Pale kijiweni (maskani) kwetu SQUAD ndo wazamiaji wengi/mabaharia walipokuwa wakitokea,wengi walizamia kwenda Italy (mfano;Salum Mnyusi aliyefia Cicily,Italy mwaka 1998),Spain,Greece,nk.Hapo story zilikuwa za Ulaya Ulaya tu,kando ya hapo ni Soka.Na wahudhuriaji wa kijiwe hiki waliokuwa wachezaji wa Simba,akina Lenny,Chumila,Masatu,Fikiri Magoso,nk walikuwa wakitupa story za soka,has a zile mechi zao za CAF walizocheza nje ya nchi.Na walikuwa wameahidi LAZIMA WAWAPIGE NKANA!Na ndivyo walivyofanya kwa kuwalamba 2 - 1 home,ingawa walienda kufungwa 4 - 1 kule Kitwe,Zambia kwenye mechi ya marudiano.Ramadhani Lenny alitueleza magoli yale 4 yalitokana na 'figisu' kibao walizofanyiwa ndani na nje ya uwanja.
NINI NATAKA KUSEMA HAPA?
1.Simba ya leo inafanana kiasi na Simba ya 1994 ila Nkana FC ya leo haifanani na Nkana ya 1994,ndo maana waliishia kuifunga Simba 2 - 1 juzi (hii si kawaida kwa Nkana wawapo kwenye "machinjio" yao ya Kitwe).
2.Kuna marekebisho machache yanapaswa yafanywe na benchi la ufundi ili kuifanya Simba ya jumapili,iwe kama/zaidi ya ile Simba ya 1994.Nashukuru kocha Patrick Aussems ameshayashughulikia mapungufu mengi ya mechi iliyopita.
3.Keshokutwa jumapili Simba itashinda na kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Kama huamini hili...rudia kusoma maelezo yangu ya utangulizi - Simba haijawahi kufungwa au kutoa droo na Nkana Red Devils kwenye home soil,na record hii itaendelezwa keshokutwa.Nkana wanaijua habari hii,na ndo maana mashabiki wao hawakufurahia matokeo yale,wachezaji wao walinyong'onyea mno,ndo maana Hassan Kessy akavaa Uzambia na kuwatia moyo wenzake (Huyu ndo alikuwa motivated baada ya mechi ukilinganisha na wenzake).
All of the best odds are with Simba,and the bad omen with Nkana FC plus their Zambian brothers from "the Desert".
Mnyamaaaaaaaaaa...👹👹👹