Kuelekea kufungua mipaka kuruhusu Watalii kuingia nchini

Kuelekea kufungua mipaka kuruhusu Watalii kuingia nchini

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,405
Reaction score
13,411
Kufungua mipaka kurusu watalii kuja ni suala mtambuka, tunahitaji utalii ni moja ya sekta kuu za uchumi katika nchi yetu (2.5 bln $ kwa mwaka 2019), lakini pia huwezi kupuuzia tishio la Corona. Kitu ambacho serikali na wadau wa utalii wanachopaswa kufanya ni kutengeneza mazingira kufanya watalii wahisi Tanzania ni sehemu salama (Takwimu za Corona ni muhimu sana katika hili). Sasa, kama wageni wataamua kuja au kutokuja ni maamuzi yao.

Lazima tukubali kwa mwaka huu wa 2020 hatutakua na namba kubwa ya wageni hata kama chanjo na dawa ikipatikana leo. Sababu Corona athari zake zimeenda hadi katika uchumi. Kuelewa hili kuna kitu kinaitwa tourism cycle elements zake kuu tatu ni tourists generating regions ( sehemu watalii wanapotokea), transit regions (sehemu watalii wanapitia kwa muda) na destination regions (sehemu wanapofikia).

Kwa utalii wetu wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na tunategemea wageni kutoka nje US, UK, Germany n.k ndio masoko yetu makuu. Ukiangalia hapa hizi nchi zote kutokana na Corona uchumi umeyumba. Na utalii si hitaji muhimu la binadamu mpaka mengine yatimie na kiasi kilichobakia ndio kinatumika kwa shughuli za utalii.

Kwa kipindi kama hiki tunaweza kuona kama ni fursa ukiangalia wapinzani wetu kwa upande wa Afrika (Kenya, Uganda na Afrika ya Kusini) zimefanya lockdown lakini tunapaswa kua makini sana na hatua zetu tunazozichukua. Sababu tusipochukua tahadhari hasara tutakazo zipata zinaweza kua kubwa kuliko faida ambazo tunaweza zipata.

Kwa maoni ili sehemu yoyote ya utalii (destination region8) iweze kusimama tena aidha wakati huu wa Covid-19 au baada. Mamlaka husika pamoja na wadau wa utalii will need to rebuild visibility, reputation, trust and communication. Njia tulizozitumia miaka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita hazitaweza kuleta matokeo yale yale.

Katika kipindi hiko utalii ulikua unakua na wadau wengi wa utalii pamoja na serikali walikua wanafanya Sales ila kipindi hiki nadhani focus inabidi ihamie katika Marketing. Ila kinachoendelea sasa hivi bado ujumbe wao ni ule ule wa kuuza. Zama zimebadilika...

960x0.jpg
 
Kuna jamaa alikua anasema watalii waliokua wamefanya booking kwake(agency) walikua wanataka daily updates za hali(Wagonjwa, vifo, wanaopona) inayoendelea hapa nchini.

Jamaa chakuwajibu hua ni kimbembe.
 
Kuna jamaa alikua anasema watalii waliokua wamefanya booking kwake(agency) walikua wanataka daily updates za hali(Wagonjwa,vifo,wanaopona) inayoendelea hapa nchini.

Jamaa chakuwajibu hua ni kimbembe.
Sababu ya availability na regular updates South Africa na Kenya zitakua first countries kupokea wageni wengi mbali ya kua ni wa mwisho kufungua mipaka. Trust! Trust! Trust and Reputation hapa ndio tunapojisahau
 
Hili sakata sijui litaishaje, kwa sisi tunaotegemea Industry ya tourism and hospitality as well kazi tunayo.

Thou we have seen the light, Wageni tayr wameanza kuja ma tunapishana nao mabatabarani. This is a sign and locus to victory

Au mnasemaje mods wa JF
 
Kuna jamaa alikua anasema watalii waliokua wamefanya booking kwake(agency) walikua wanataka daily updates za hali(Wagonjwa,vifo,wanaopona) inayoendelea hapa nchini.

Jamaa chakuwajibu hua ni kimbembe.
Sababu ya availability na regular updates South Africa na Kenya zitakua first countries kupokea wageni wengi mbali ya kua ni wa mwisho kufungua mipaka. Trust! Trust! Trust and Reputation
Hili sakata sijui litaishaje, kwa sisi tunaotegemea Industry ya tourism and hospitality as well kazi tunayo.

Thou we have seen the light, Wageni tayr wameanza kuja ma tunapishana nao mabatabarani. This is a sign and locus to victory

Au mnasemaje mods wa JF
Sign ipo nchi zishaanza kuruhusu kurudi makazini na wale wenye savings zao watapenda kutalii sehemu mbalimbali tutegemee nasi kupata share yetu ingawa itakua kiduchu sana
 
Back
Top Bottom