Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,284
Reaction score
38,364
Binafsi nilijiandikisha tena mara mbili lakini nimefuatilia namba zangu NIDA kama naomba mkopo benki. Hakuna nilichoambulia. Uzembe wa NIDA usumbufu nabebeshwa mimi.

Matokeo yake naambiwa nijiandikishe upya, yaani nianze taratibu za kwenda kwa Mtendaji, Uhamiaji halafu NIDA.

---
Mambo ya msingi ya kufanya kabla ya laini kufungwa kama huna namba ya kitambulisho cha NIDA


---
Dakika chache kutoka sasa simcard zisizosajiliwa zitazimwa



---UPDATE 21 January, 2020---
TCRA kufungia laini zisizosajiliwa kwa awamu


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema uzimaji wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole unafanyika kwa awamu

Amesema zoezi hilo lililoanza jana Januari 20, 2020 linafanyika kwa awamu ili kuondoa usumbufu na hadi kufikia jana usiku saa nne walikuwa wamezima laini 975,041

Amesema kundi la kwanza waliozimiwa laini ni watu 656,091 ambao wana Vitambulisho vya Taifa au namba lakini hawajasajili laini zao

Amebainisha kuwa kundi la pili ni watu 318,950 waliosajili laini zao kwa Kitambulisho cha Taifa kabla ya kuanza mfumo wa kusajili kwa alama za kidole

Amesema, “Tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja kwa maana watajazana kwenye kusajili kitu kinachofanya mifumo ya Nida inaelemewa.”
 
Nilikuwa sina mpango wa kusajili line yangu ya simu ingawa sina sababu ya msingi kabisa NIDA ninayo ile ya mwanzo kabisa ya yule aliyeshitakiwa basi tuu sikuwa nataka usumbufu ila nadhani sasa naweza sajili
 
Nilikuwa sina mpango wa kusajili line yangu ya simu ingawa sina sababu ya msingi kabisa NIDA ninayo ile ya mwanzo kabisa ya yule aliyeshitakiwa basi tuu sikuwa nataka usumbufu ila nadhani sasa naweza sajili
Wewe unaweza kuwapigia wale wanaosajili line mtaani wakakusajilia hata Nyumbani kwako, hongera umeyapatia Maisha. [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unaweza kuwapigia wale wanaosajili line mtaani wakakusajilia hata Nyumbani kwako, hongera umeyapatia Maisha. [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app


Yaani nimecheka kwa sauti ya juu hapo kwenye kupatia maisha ... Mkuu bado sema mimi kipindi kile cha kujiandikisha NIDA sikuukataa wito nilifanya hivyo kwa siku tatu mfululizo mpk kuja kufikia sehemu ya kupiga picha nakumbuka nikaenda halafu nikachana na hiyo biashara nikaja kutumiwa msg sijui baada ya miezi zaidi ya minne nikafuata kitambulisho.


Mimi huwa sina tabia ya kupuuzia mambo huwa nasema ngoja nifanye ikae hapo huwezi jua....
 
NIDA kumekuwa na folen ya kufa mtu sio kwa kuwa watu wanataka vitambulisho vya Taifa bali kwa kuwa wanapigania namba zao za simu zisizimwe

Yaan watu hawana mpango na vitambulisho sema tu inabidi wawe nacho kukamilisha usajili

I.e line ya simu ni muhimu kuliko kitambulisho
ikitangazwa kuwa usajili wa line sio muhimu kitambulisho cha NIDA basi folen inaisha fasta
 
Poleni sana mtakaozimiwa line! Ni muhimu kufanya jambo kwa wakati sahihi na kwa muda sahihi si vizuri Sana kila Jambo ufanye dakika za mwisho/dakika za lala salama.

Usikate tamaa bado muda upo na usiruhusu hali ya kuupuza vitu, uvivu au uzembe ukutawale.
 
Kajiongeze kwa wale mawakala watakufanyia mchakato
 
Poleni third world dwellers yani mnatawaliwa na misomi uchwara yenye PhD uchwara
 
Kisaikolojia fanya haya. Kama una smartphone utaendelea na internet kwa wi fi ya mtu mwingine karib. Utaacha aina zote za mikopo ya mitandaon. Utafanya mawasiliano ya kupiga kwa internet tu bila line kwenye whasapp, viber etc. Utarudia mifumo ya kibenk kuhusu pesa hasa huduma ya cardless. Mwisho wa yote utaambulia usumbuf kias lakin kampun zitapoteza makato meng yanayokuhusu na serkali itapoteza mapato ya kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…