Kuthibitisha kama laini yako ya simu imesajiliwa kwa alama za vidole piga *106# chagua 1
Kwanza niwape pole wale wote ambao wanashinda ofisi za NIDA bila kufanikiwa.
Ukweli process ya vitambulisho ni ndefu sana.
Kwa wale ambao hawana vitambulisho vya NIDA unaweza tafuta ndugu yako ukasajili kwa kutumia kitambulisho chake, kitambulisho kimoja kinaruhusiwa kusajili laini 10.
Kwa wale ambao hawajasajili hakikisha fedha zote umezitoa na kama umezoea kutumia mobile banking hakikisha kadi yako ya ATM ipo valid otherwise utapata usumbusu mkubwa sana kupanga foleni bank na kupata ATM mpya inachukua more than one week.
Kwa NIDA nashauri watume majina na namba za wananchi ambao wameshajaza form na hawajapata namba zao ili mitandao ya simu (MNO) wasiwafungie kwa sababu hawana hatia.
Nawatakia weekend njema.
------
Waziri Nditiye asema hekima itatumika usajili wa laini kwa wasio na vitambulisho vya Taifa
Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.
Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.
"Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,β amesema Nditiye.
Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.
Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.
Chanzo: Mwananchi
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa inaendelea na zoezi la usajili na utambuzi wa watu, uzalishaji wa namba za utambulishi wa taifa na vitambulisho na ugawaji wake kwa wananchi ili waweze kuvitumia kusajili kadi (laini ) za simu kwa alama za vidole na huduma nyingine. Katika...