Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
Na Twahir Kiobya (The Man)
Kipyenga cha nafasi ya uwenyekiti katika chama cha CHADEMA kimeshalia, na tunaambiwa kuwa kutakuwepo mdahalo wa wazi baina ya wagombea wa nafasi hiyo yaani Tundu Lissu na Freeman Mbowe.
Hili ni jambo zuri maana linatoa fursa kwa wagombea kueleza malengo, dhamira na sera zao za kukitoa chama hapa kilipo na kukipeleka hatua nyingine.
Leo tutizame nguvu ya kila mmoja ktk ushawishi na kuvutia uungwaji mkono
NGUVU ZA LISSU
1. THE FIERCE UNDERDOG.
Watanzania wanapenda underdog mpambanaji, wanapenda underdog mbishi. Hii ni kwa sababu inaakisi haiba yao, wanachukia mambo mengi ila hawana ujasiri wa kusimama kuyakabili. Akitokea mtu mmoja mbishi, jasiri na mwenye integrity wa kupambana na mfumo huwa wanamuelewa sana. Ilikuwa hivyo kwa Nyerere dhidi ya muingereza, Mrema dhidi ya CCM, Mtikila na hata yeye Lissu dhidi ya Magufuli. Hata hivyo hii huwa na time-frame, hawataki uwe underdog "milele" maana inatoa ishara kuwa wewe ni loser. Katika kinyanganyiro hiki cha uenyikiti, Lissu anaingia kama underdog dhidi ya Mbowe, Mwenyekiti powerful mwenye mizizi iliyojikita ndani ya mifumo ya chama. Lissu akijua jinsi ya kuitumia nguvu hii atapata advantage kubwa sana ktk kuwashawishi wanachadena na umma uwe upande wake.
2. TASWIRA YA MABADILIKO
Lissu anakuja na Taswira mpya ya mabadiliko inayoclick na watu wengi ndani na nje ya CHADEMA. Kwa mujibu wa sensa ya miaka takriban mitatu iliyopita, Vijana wana asilimia kubwa ya Idadi. Wengi wao tangu wakiwa watoto wanamuona Mbowe tu na kombati lake maana kakaa madarakani kwa miaka 20, wanaona sura ileile kila siku. Watu wanataka mabadiliko, wanataka mawazo mapya, utendaji mpya. Mtu anazaliwa fulani ni mwenyekiti, halafu mtu huyo anakuwa mkubwa hadi anamaliza chuo kikuu fulani bado ni mwenyekiti!, umekuwa SULTANI?
3. LISSU ANA KITU CHA KUONYESHA KUWA NI WAKALA WA MABADILIKO
Historia inamhukumu vizuri Lissu. Tangu akiwa kijana mbichi ametumia vipawa vyake, nguvu zake, ujasiri wake kutetea watu. Alifanya hivyo kutetea wachimbaji wadogowadogo huko Bulyanhulu Shinyanga, Nyamongo Tarime enzi za utawala wa Mkapa na akaendelea kutetea jamii ya Wamasai wa Ngorongoro. Pia ana historia ya kutetea watu mahakamani kama wakili bure!. Hili jambo limemjengea heshima na mapenzi makubwa ya watu wa jamii hizo. Ndiyo maana wajumbe wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali nchini wanamkubali
4. LISSU ANA MAKOVU YA KUONYESHA KUWA AMEZIISHI STRUGGLES KWELIKWELI.
Lissu amefunguliwa kesi nyingi tangu utawala wa BWM. Amesurvive risasi 16, Akajivika ujasiri na kutoka kwenye matibabu kuja kupambana na JPM kwenye uchaguzi wa 2020, licha ya maumivu ya mwili na risasi bado ingali mwilini lakini jamaa kapanda ndege kuja kupambana na JPM kwenye uchaguzi. Huyu si mtu wa kubeza ujasiri wake ktk struggle.
5. LISSU BINGWA WA USHAWISHI KWA KUTUMIA LOGOS
Mwanafalsafa Aristotle alisema kuna njia kuu tatu za ushawishi ktk hoja, Logos, Pathos Ethos. Yaani kushawishi watu kwa logic (logos), kushawishi watu kwa status ya mtu katika jamii (Ethos), na kushawishi watu kwa Pathos (kutumia emotions). Katika mbinu zote hizo Lissu amemaster uwezo wa kushawishi watu kwa kutumia mantiki, kufundisha, kudadavua n.k. Hili limefanikiwa kumfanya aeleweke sana.
6. ZIARA ZA KUZUNGUUKA MIKOANI ZIMEMJENGA SANA LISSU
Tangu alipogombea urais mwaka 2020, Lissu kazunguuka sehemu nyingi nchini, anafahamika mbele ya wananchi na Wanachadema. Ziara na operesheni mbalimbali za kuzunguuka mikoani mwaka jana tena kwa gari, kituo kwa kituo kumemfanya Lissu afahamike na hii imempa connection kubwa mbele ya umma, Japo ktk kinyanganyiro hiki na mwenyekiti yeye ni underdog lakini ni underdog mwenye kufahamika sana. Hili linampa faida kubwa.
7. LISSU ANAZUNGUMZA MAMBO YANAYOKUBALIWA NA WANACHADEMA WENGI
Lissu anapozungumza nia yake ya kuweka ukomo kwenye ubunge wa viti maalum, Wanachadema wengi akina mama wanamuelewa sana. Siyo mtu anakuwa mbunge wa viti maalum miaka 10, ina maana miaka yote hiyo hujakomaa tu?
Lissu anapuzungumzia, pesa za ruzuku kiasi kikubwa kisiishie makao makuu tu, hiyo pia inaclick na wajumbe wengi wa ngazi za chini maana haiwezekani wanajitoa sana kujenga chama lakini usaidizi wa kipesa ni mdogo sana ila mipesa mingi inabaki huko juu makao makuu. Baadhi ya haya mambo yanafanya wanachadema wamuone kuwa kweli huyu mtu anakuja na agenda ya reforms inayomake sense.
MADHAIFU YA LISSU
1. Lissu ANA ARROGANCE (KIBURI FULANI) KINACHOKERA.
Ninatambua, kuwa Kuna msitari mwembamba sana kati ya ujasiri na kiburi. Wakati mwingine mwingine Lissu huvuka msitari huu na kuonyesha arrogance. Hii hujitokeza kwenye aina ya maneno anayochagua kwa mfano kumuita JPM "Dikteta uchwara", Kusema maneno kuwa "Huyu siyo mama yangu, hajanizaa", "Fulani ni dalali", "Hayo ni maneno ya kijinga". Ni baadhi ya kauli za Lissu. Hii hali huwa inawaput off watu wengi, kama anataka ushawishi inabidi apunguze ukali wa maneno yake.
2. NI BINGWA WA LOGOS ILA NI DHAIFU KWENYE KUTUMIA TAKWIMU.
Licha ya uwezo wake wa kujenga hoja kwa kutumia Mantiki (Logic), Lissu huwa ni dhaifu sana kwenye kurejea takwimu. Ni mara chache mno kumsikia akinukuu hali ya umasikini wa watu na mambo mengine yanayohusu maisha ya wananchi kwa takwimu. Kama anataka kuongeza ushawishi wake siku ya mdahalo hili eneo la takwimu lazima alifanyie kazi. Zitto Kabwe ni mzuri sana wa kujenga hoja kwa kutumia takwimu, Lissu anaweza kuupdate ushawishi wake kwa kufanyia kazi hili.
3. KUNA MISIMAMO ALIIWEEKA HUKO NYUMA KUGEUKA KWAKE KUNAMUONDOLEA CREDIBILITY.
Baada ya uchaguzi mkuu uliopita alitumia muda mrefu kuwafundisha watu kuwa haiwezekani kuwa na uchaguzi wowote credible, wa haki chini ya katiba ya sasa na sheria hizi za uchaguzi. Akatoa kauli maarufu kuwa kushiriki chaguzi hizi kwa katiba hii ni UKICHAA Lakini baadae kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa alionekana akitetea kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa ni jambo zuri sana licha ya kutokuwepo mabadiliko ya msingi ktk katiba na sheria zinazosimamia uchaguzi. Na yeye mwenyewe alikiri kuwa Hivi karibuni wamewachanganya sana Watanzania. Sasa huwezi kuwachanganya Watanzania credibility yako ikabaki vilevile.
Lissu ndiye aliyeshiriki kwa kiwango kikubwa kuandika waraka wa List of Shame, waraka uliowataja watu mbalimbali kuwa ni mafisadi. Baadae Lissu huyohuyo akawana ni miongoni mwa vinara vya kumnadi mgombea mmoja kupitia chama hicho ambaye Lissu alimuita Fisadi. Baadae Lissu anajitetea kuwa mtu huyo ufisadi uliisha baada ya kuwajibika kwa kujiuzulu nafasi yake. Huu ni utetezi dhaifu kwa sababu mtu huyo hakutajwa kwa tuhuma moja tu ndani ya waraka wa list of shame, alitajwa kwa tuhuma nyingi tu ambazo hakuwahi kuwajibika nazo na pia akina Lissu waliendekea kumuita fisadi licha ya kuwa alikuwa amejiuzulu nafasi yake. It is only alipokuja kugombea kupitia chama chai ndo waliacha kumuita fisadi na kuanza kumsafisha mbele ya umma. Utetezi mwingine anaotoa Lissu eti yule bwana alileta wabunge wengi na madiwani wengi chadema. Hiyo siyo hoja kwa maana ubunge wao kwanza haukuwa wa kusimamia misingi ya upinzani nchini na wala haukuwa rooted ktk misingi ya Chadema ndiyo maana Yule bwana aliporudi CCM na watu wake wakarudi hukohuko. KIUFUPI Lissu na wenzie walikuwa wanatafuta shortcut ya kuingia Ikulu bila kujali cost ya kufanya hivyo na bila ya kusimamia misingi thabiti ya kufanya hivyo. Yaani kuireplace CCM kwa CCM.
LISSU ANACHOTAKIWA KUFANYA KUANZIA SASA HADI MDAHALO
1. Atambue kuwa Watu wamemuelewa sana ila Watu wanaipenda Chadema zaidi
Nimefuatilia comments za watu mitandaoni, Lissu akiongea wanaonyesha muitikio chanya ila wanapohisi kuwa anachoongea kinaenda too far kuhatarisha maslahi ya Taasisi ya CHADEMA kunakuwa na pushback/rebuke kubwa sana dhidi yake kutoka kwa watu. Lissu ajitahidi kuongea kwa tone itakayowahakikishia watu kuwa move yake ni kwa maslahi ya chama zaidi na si tu kwamba anagombea for the sake ya kupambana na mwenyekiti. Lissu awahakikishie watu kuwa akishinda itakuwa ni heri kwa chama, na akishindwa hatokuwa chanzo cha kuibomoa CHADEMA.
2. LISSU aelewe kuwa Humble appearance ya Mbowe ni Strength na silaha kubwa ya Mbowe.
Ni kweli watanzania wanapenda underdog, lakini hawapendi underdog arrogant. Mbowe moja ya strength yake ni kujiposture kama muungwana sana. Lissu inambidi amtreat Mbowe kiuungwana, inabidi aonyeshe mapungufu yake kwa unyenyekevu mkubwa, asishambulie haiba ya mwenyekiti maana haiba ya mwenyekiti ina quality ambayo watu wanaipenda. Inabdi ashawaishi watu kuwa mwenyekiti sasa hatoshi. Inabidi ampe credit mwenyekiti kwa mazuri kadha wa kadha aliyofanya. Akifanya hivyo ataonekana muungwana.
3. Siku ya Mdahalo inabidi aongee na nyoyo za watu siyo Intellect peke yake.
Badala ya kutumia Logos peke yake, itabidi achanganye na Pathos (appeal to emotion). Ukiappeal kwa intellect peke yake, effect huwa ni short lived, ila ukiappeal kwa emotions effect yake hukaa muda mrefu. Lissu ahakikishe anagusa emotion triggers za Wanachadema na wananchi siku ya mdahalo wake. Na offcourse asisahau kufanyia kazi takwimu kama nilivyoeleza hapo juu
4. Siku ya mdahalo asisahau personal appearance, shave, avae kimamlaka, akeep cool, comfortable, humble, wise na akeep tone yake isiwe kama anarant bali anadebate.