Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Klabu ya Simba SC kufika hatua ya robo fainali ya CAFCL na CAFCC siyo jambo la kushangaza, ni kawaida tu, ndiyo maana malengo ya Klabu kwa sasa ni Nusu Fainali na Fainali na ikiwezekana Ubingwa. Na mechi rahisi ni ile ambayo imetamatika kwa kufikia malengo na si kwa fikra.
Kuelekea mechi ya CAFCC dhidi ya Orlando Pirates April 17, 2022 saa 1:00 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa. Ni hatua mbili ngumu na muhimu sana kwa Simba SC kwenye kufikia malengo ambayo yamewekwa na Klabu, hivyo basi tuelekeze maoni yetu Wanasimba na Wadau wa Kabumbu kwenye benchi la ufundi na Wachezaji pamoja na Viongozi katika kuandaa timu ya kuvuka hatua hii muhimu na ngumu, kwani mpira wa miguu ni mchezo wa hisia, akili, nguvu na kujiandaa Kisaikolojia.
1. Kucheza kwa ubora Nyumbani na Ugenini, huku kila mchezaji akicheza kwa kujituma zaidi kwa kuthamini nembo ya Klabu.
2. Kujua namna ya kucheza mechi za mtoano, kuwa na mbinu zote muhimu, 'Na ndo maana Waarabu kwenye michuano ya CAF, wanaamini kuwa mechi kubwa kwao ni mbili tu, hatua ya Mtoano na Fainali'.
3. Kucheza kwa kumfikiria zaidi mpinzani unayecheza naye, kwa kumheshimu kuwa amekuja kutafuta matokeo ya ushindi huku ukiwa na akili pevu kuwa anaweza kufanya lolote shughuli ikaishia hapo.
4. Kuwa na utimamu sahihi kucheza mchezo huo, kuacha Uzembe na Kubweteka ili kupatikane ile TeamWork.
Pamoja na Ufundi na Mbinu ya Kocha Pablo Franco Martin, haya ndo yakuelekezwa kwenye mchezo huu muhimu na mgumu sana, huku tukiamini kuwa tumefika hatua hii ni kwakuwa Simba SC wapo njia sahihi kwenye ukubwa wa CAF.
Orlando Pirates wanakaribia kuvuta pumzi ya moto haswa kutoka kwa Simba SC Mnyama Mkali Mwituni kama waliovuta wale waliotamgulia
Kulipewa Mwana....Kulitaka Mwana.