Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kuelekea patashika ya ligi kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL), nyasi za Uwanja wa Kaitaba Stadium, mkoani Kagera kuwaka moto ambapo leo September 26, 2019 Kagera Sugar, Wana Nkurukumbi, wanawakabili vilivyo Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, kutoka jijini Dar es salaam.
Mchezo huu kati ya Kagera Sugar na Simba SC, una vuta hisia za wapenda kandanda kote nchini, hivyo basi unatarajiwa kuwa mkali na wenye kusisimua kwa muda wote wa dakika tisini, kutokana na rekodi za timu hizi mbili hivi karibuni zinapokutana.
Kocha Patrick Aussems, amesema safari hii hawachomokei na amedhamiria kuondoka na alama tatu muhimu, huku akiongeza kuwa;
"Yaliyotokea msimu uliopita ni hamasa kwa wachezaji kufanya vizuri kuelekea mchezo huu, na nimeshawaambia kwamba lazima tuwaonyeshe kuwa sisi ni Simba SC". alisema Kocha Aussems.
•••Usikose Ukaambiwa, kuhusu burudani ya kandanda itakayovurumishwa kwenye dimba la Kaitaba Stadium. Kumbuka kipute hiki ni kuanzia saa 10:00 jioni.
•••Wamezoea Lakini Leo Hii Tunao