Kuelekea mechi ya watani wa jadi, kipi unakikumbuka katika historia ya Klabu hizi?

Kuelekea mechi ya watani wa jadi, kipi unakikumbuka katika historia ya Klabu hizi?

Lee

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
43,973
Reaction score
150,463
SIMBA na YANGA ni timu zenye historia kubwa katika mpira wetu wa Tanzania tokea kuanzishwa kwake mpaka muda huu japo yawezekana historia ya klabu hizi haiendani na maendeleo ya hizi timu kwa ujumla

Kwa miaka ya hivi karibuni SIMBA zamani ikijulikana kama SUNDERLAND wazee wa lunyasi , wazee wa pira biriani wamekuwa na hali nzuri ya timu yao hasa baada ya kuanza utaratibu wa kufanya transformation ya club

Yanga hawako nyuma wanapambana kufanya mabadiriko ili kuendeleza ushindani, yapo matokea na matukio ambayo yametikisa hizi mechi maarufu kama watani wa jadi .

Yafautayo ni baadhi na wanajamvi tujikumbushe matukio na matokea ya mechi za nyuma
1.

NOVEMBA 9, 1996
Yanga v Simba
4-4
WAFUNGAJI:
Yanga: Edibilly Lunyamila (penalti) dk. 28, Mustafa Hozza alijifunga dk 64, Said Mwamba 'Kizota' dk. 70, Sanifu Lazaro dk. 75.
Simba: Thomas Kipese dk. 7, Ahmed Mwinyimkuu dk. 43, Dua Saidi dk. 60 na 90.
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha)

2.
MEI 1, 1999
Yanga v Simba
3-1
WAFUNGAJI:
Yanga: Idd Moshi dk. 59, Kalimangonga Ongala dk. 64, Salvatory Edward dk. 70, Simba: Juma Amir d

3.
AGOSTI 29, 1999
Yanga v Simba
2-0
WAFUNGAJI: Bakari Malima dk. 49, Mohamed Hussein 'Mmachinga' dk 71
4.
JUNI 25, 2000
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Steven Mapunda dk. 59 na 72
Yanga: Idd Moshi dk. 4.
5.
SEPTEMBA 1, 2001
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Joseph Kaniki dk. 76
6.

SEPTEMBA 30, 2001
Simba v Yanga
1-1
WAFUNGAJI:
Simba: Joseph Kaniki dk. 65,
Yanga: Sekilojo Chambua dk. 86
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza)

7.

AGOSTI 7, 2004
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Shaaban Kisiga dk. 64, Ulimboka Mwakingwe dk. 76
Yanga: Pitchou Kongo dk. 48
8.
SEPTEMBA 18, 2004
Simba v Yanga
1-0
MFUNGAJI: Athumani Machuppa dk. 82
9.
APRILI 17, 2005
Simba v Yanga
2-1
WAFUNGAJI:
Simba: Nurdin Msiga dk. 44, Athumani Machupa dk. 64,
Yanga: Aaron Nyanda dk. 39
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)
10.
AGOSTI 21, 2005
Simba v Yanga
2-0
MFUNGAJI: Nico Nyagawa dk. 22 na 56
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha)
11.
MACHI 26, 2006
Simba v Yanga.
0-0
12.
OKTOBA 29, 2006
Simba v Yanga
0-0
JULAI 8, 2007
13.
Simba v Yanga
1-1 (dakika 120)
WAFUNGAJI:
Simba: Moses Odhiambo (penalti dk. 2)
Yanga: Said Maulid (dk. 55).
(Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare hiyo).
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)

OKTOBA 24, 2007:
Simba Vs Yanga
1-0
Mfungaji: Ulimboka Mwakingwe
(Mechi hii ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro)
14.
APRILI 27, 2008:
Simba Vs Yanga
0-0
15.
OKT 26, 2008
Yanga Vs Simba
1-0
MFUNGAJI: Ben Mwalala dk15.
(Mechi hii ilichezwa Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam)

16.

APRILI 18, 2010
Simba Vs Yanga
4-3
WAFUNGAJI:
SIMBA: Uhuru Suleiman dk 3, Mussa Mgosi dk 53 na 74, Hillary Echesa dk 90+
YANGA: Athumani Iddi dk 30, Jerry Tegete dk 69 na 89
17.
OKTOBA 16, 2010:
Yanga Vs Simba
1-0
MFUNGAJI: Jerry Tegete dk 70
18.
MACHI 5, 2011
Simba Vs Yanga
1-1
WAFUNGAJI:
YANGA: Stefano Mwasyika (penalti) dk 59.
SIMBA: Mussa Mgosi dk 73.
(Refa Orden Mbaga alizua tafrani uwanjani, kwanza kwa kulikataa bao la kusawazisha la Simba, kisha akalikubali baada ya kujadiliana na msaidia wake namba moja).
19.
OKTOBA 29, 2011
Yanga 1-0 Simba
MFUNGAJI: Davies Mwape dakika ya 71

20
MEI 6, 2012
Simba 5-0 Yanga
WAFUNGAJI:
Emmanuel Okwi dk 1 na 65, Patrick Mafisango pen dk 58, Juma Kaseja pen dk 69 na Felix Sunzu pen dk 74
 
Ile ya penalt hiyooo!
Penalt hiyoo!
Simba yakina
Singano
Ndemla
Mkude
Wiliam lucian nawakongwe kina
Cholo
Tambwe
Kaze gilbet
Owinogera
Na jamaa m1 cjui ashapotelea wapi huyu
Betram mwombeki!
Mwisho uto 3-3 lunyasi
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Nakumbuka siku ya Mechi ya kwanza Kabisa ya Uwanja wa Taifa kwa sasa Ukiitwa Lupaso kwa MKAPA mara paaaap siku ikafika. Wazee, Vijana na akina Mama tukaijaza LUPASO tooop kujionea nani atakuwa mbabe wa Taifa kwa mara ya kwanza. Kama Kawaida Simba tulijaaa tele na Uzi wetu mwekundu.
Ayseee Vyura wakatupiga Kimoko mpaka dkk 90 zinaisha,nadhani Mtupiaji alikuwa BEN MWALALA au Boniphace Ambani. Niliumia sana, nilipenda SIMBA ndio wawe na Historia ya kushinda gemu ya kwanza hapo Lupaso lkn haikuwa hivyo.
All in All Simba kesho Pointi 3 tuendelee kujipanga na gemu ya Kaizer Chiefs, Pia NINJA ajiangalie hizo judo zake atakula Umeme.
 
Nakumbuka na kulienzi tukio moja tu. Madaraka Suleiman mzee wa kiminyio alivyoituliza begani ile ngoma alafu akatikisa nyavu,kuna shabiki wa Yanga alianguka chini ghafla tukaanza kumpepea kwa mashati.

Jamaa baada ya kuzinduka akatoka nduki watu wakamkamkamata asikimbie,,akaulizwa"unakwenda wapi',,akasema naenda kaburini bola nife tu kuliko haya mateso ninayopata.
Hiyo mechi Yanga walikula'KHAMSA.
 
Kuna mechi ilichezwa usiku Zanzibar miaka ya 70, Yanga iliifunga Simba 2 bila. Naomba wahenga akiwemo Mzee Said tukumbushane ilikuwa mwaka gani na kikosi kilichocheza siku hiyo.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Nakumbuka na kulienzi tukio moja tu. Madaraka Suleiman mzee wa kiminyio alivyoituliza begani ile ngoma alafu akatikisa nyavu,kuna shabiki wa Yanga alianguka chini ghafla tukaanza kumpepea kwa mashati.

Jamaa baada ya kuzinduka akatoka nduki watu wakamkamkamata asikimbie,,akaulizwa"unakwenda wapi',,akasema naenda kaburini bola nife tu kuliko haya mateso ninayopata.
Hiyo mechi Yanga walikula'KHAMSA.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwenye tarehe kama ya leo hizi timu zimekutana mara nne kama kumbukumbu ziko vizuri

Yanga ikishinda mechi ya kwanza kwa mara ya kwanza november 8 ,1997 yanga ikishinda 1-0

Ya pili july 8,2007 dk 90 1-1 ila simba akashinda kwa penet

March 8 ,2015 simba akatoboa 1-0

Ya hivi karibuni ni ile ya mzee wa kukera ni ya march 8, 2020 yanga anatoka kifua mbele 1-0
 
Kuna siku watu waliogopa kupeleka timu uwanjani wakaishia njiani 😂😂 ilikuwa ni kagame cup mwaka 2007/08 kama sikosei
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kuna siku watu waliogopa kupeleka timu uwanjani wakaishia njiani [emoji23][emoji23] ilikuwa ni kagame cup mwaka 2007/08 kama sikosei
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] kwani leo hawaogopi?
 
Back
Top Bottom