Kuelekea mpambano wa Watani wa Jadi, Simba atafungwa Goli 3-0

Yanga zote mbovu.
Yanga ya gsm Shaban Juma,Mayele na Yanick Bangala ilicheza na Zanaco ikapigwa mbili.
Yanga ya Dr.Msola Yacouba,Kibwana Shomari na Mauya ilicheza na Rivers ikapigwa mbili nje ndani.
Ni simba gani ilifungwa na Tp mazembe?
 
Ni simba gani ilifungwa na Tp mazembe?
Mazembe sio Yanga.
Mazembe kwa ukubwa wake alikua na haki ya kuifunga Simba hata goli tano.ni haki yake Mazembe kuifunga Simba kwasababu sifa na ubora wa Mazembe upo juu zaidi ya Simba.

Lakini sifa na ubora wa Rivers ni wa chini sana kiasi kwenye CAF ranking River ni ya nne kutoka chini.mmefungwaje na wale madogo nyinyi?
 
Hahaha nipe rekodi za matokeo ya simba na Yanga kwa misimu 3 nyuma mfululizo kwenye ligi kuu Tanzania bara
 
Kwahiyo Simba ikifungwa na Yanga utatoa mlinganisho upi baina ya Simba na Yanga?
 
Hahaha nipe rekodi za matokeo ya simba na Yanga kwa misimu 3 nyuma mfululizo kwenye ligi kuu Tanzania bara
Rekodi zipo na nazijua,kabla atujahama mada kwanza umeelewa somo nililokupa?
 
Kwahiyo Simba ikifungwa na Yanga utatoa mlinganisho upi baina ya Simba na Yanga?
Simba ya sasa ni bora kuliko Simba zote na haitotokea Simba ya sasa ikafungwa na Manyani f.c,never.
 
Simba ya sasa ni bora kuliko Simba zote na haitotokea Simba ya sasa ikafungwa na Manyani f.c,never.
Mimi naomba unipe jibu ikitokea Simba kafungwa na Yanga je Simba itakuwa ni mbovu?
 
View attachment 1949461

Akili za Manara hizo!
 
Upo sahihi mkuu /simba msisahau kuja na paka walao
 
Sitashangaa maana yanga wao wanajua mpira ni kuifunga simba tu.
 
Mechi ya mwisho Simba na Yanga inajulikana nini Yanga kilimpata kombe likiwa uwanjani.
Hatuzungumzii ushindi wa CHOPRICHOPRI, tunazungumzia ushindi wa wanaume wametimia uwanjani na sio ule wa kuwapunguza idadi wapinzani uwanjani ndo mnashinda
 
Hatuzungumzii ushindi wa CHOPRICHOPRI, tunazungumzia ushindi wa wanaume wametimia uwanjani na sio ule wa kuwapunguza idadi wapinzani uwanjani ndo mnashinda
Kilichofanya mpungue ni ushamba wa mchezaji wenu kucheza kung-fu uwanjani.kilasiku mnaambiwa sajili wachezaji sio wakulima.
 
Kama kocha wa Simba atapanga yale ma-double striker yake yasiyokuwa na tija na kuwaweka bench Banda na Sako, siioni Simba kutoboa. Huko kutakuwa ni kuuwa vipaji vyao kama alivyofanya kwa Chikwende ambaye naamini ni mchezaji mzuri tu.
Yanga wana fungika kiurahisi sana na wachezaji wanyumbulifu na kina Mugalu and the like.
Na ninaamini hakuna striker yoyote yule wa Simba atakayefikisha magoli kumi msimu huu kwani mpishi wao CCC hayupo tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…