Tunapoelekea katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, hali inazidi kuwa ya kushangaza. Jana na leo, hoteli na nyumba za kulala wageni zimejaa – lakini si kwa ajili ya ibada au tafakari, bali kwa matendo machafu. Wengine wanajihusisha na uzinzi wakidai wanajiandaa kwa mfungo, jambo linaloleta maswali mengi kuhusu nia na maadili yao.
Pia, kuna tabia mpya ambapo baadhi ya watu wanafunga ndoa kwa haraka, wakijidai kutafuta uhalali wa mahusiano yao kwa muda wa mwezi mmoja. Mara tu Ramadhan inapomalizika, ndoa hizi zinavunjika kama hazikuwahi kuwepo. Je, haya ni maandalizi ya mfungo au ni unafiki wa hali ya juu?
Tuwashangae wanaofunga nini? Mfungo wa Ramadhan unapaswa kuwa kipindi cha kujitakasa, si kufunika dhambi kwa hila. Ni wakati wa kutafakari na kujirekebisha, sio kufanya maovu kisha kujifanya watakatifu.