Kuelekea mwezi mtukufu wa RAMADHAN

Kuelekea mwezi mtukufu wa RAMADHAN

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Mbunge mmoja nchini Uingereza atangaza kufunga suamu ya Ramadhani wiki moja kwa lengo la kujifunza hali ambayo huwa nayo waislamu kipindi hicho.

Mbunge mmoja nchini Uingereza ametangaza kufunga swaumu ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa muda wa wiki moja akiwa na lengo la kutaka kufahamu ni jinsi gani waislamu hujisia wakiwa katika ibada ya hiyo ya funga.

Kama inavyofahamika, swaumu ya mwezi Mtukufu wa Rmadhani ni kujizuia kula, kunywa na mambo mengine ambayo hayamoendezi Mwenyez Mungu kwa muda wa mwenzi mmoja.

Paul Bristow amesema kwamba atajaribu kufunga na baadae kufahamisha alivyojisikia.

Katika video yake aliorusha katika ukurasa wake wa Twitter, Paul Bristow amesema kuwa anataka kufahamu maana na umuhimu wa Ramadhani kwa waislamu baada ya kuwaona wakiwa na masikitiko kutokana na zuio la kutotoka nje lililosababishwa na virusi vya corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom