Yousuph .M.
Senior Member
- Apr 16, 2011
- 123
- 24
Wadau,
Ninae mchumba ambae natarajia inshallah kumuoa na sote tumeridhiana, cha ajabu ndg zangu wa karibu hapo awali waliridhia na kushinikiza nimuoe lakini kwa siku za karibuni hao dada zangu wameanza kufitini chini kwa chini kwa kuwajaza maneno wazazi wangu eti 'wasiridhie' na kuanza kutoa vigezo visivyo na mantiki. Ajapo kwangu huyo mchumba...huwa wako tofauti sana na hawamchangamkii kabisa na kuonyesha kutokumkubali, huku sms zikitawanywa na hatimaye kunifikia.
Hapo nyuma huyu mchumba wangu alikuwa ni swahiba mkubwa wa dada zangu, na urafiki wao huo ulianza baada ya mie kuwapa introduction ndipo wakashamiri kiurafiki. Sasa, kuna kila dalili za dada zangu kuanza fitna kwa wazazi ili wasiridhie juu ya suala langu hili la kindoa, ilhali nimesharidhia kwa yote muhimu niliyoyahitaji toka kwa mtarajiwa wangu, na nimekuwa nae kwa takriban miaka miwili.
Naomba ushauri wenu wadau,