Mawifi wengine bana, usikute wameanza kumchukia sababu tu, waliomba labda kitu fulani wakanyimwa, au zamani ulikuwa unawashirikisha kwenye vitu vyako na sasa huwashirikishi tena na hauwashirikishi si sababu hawapendi dada zake hapana, kapata mtu wa karibu wa ku share nae vitu muhimu kuhusu maisha
Hapo kijana unatakiwa uwe na maamuzi mazito,waite ukae nao kitako uwaulize ni nini kimewachukiza ukiweke sawa na uendelee na mpenzi wako, ndugu wanaweza wakakufanya ushindwe kuishi na mpenzi wa maisha yako, usiwape nafasi waeleweshe kwamba huyo ndio umemchagua awe mkeo. Wazazi siku hizi hawafatilii mambo kama hayo wanawaacha watoto watafute wenyewe wachumba zao