Kuelekea Ngao ya Jamii Simba SC Vs Yanga SC

Kuelekea Ngao ya Jamii Simba SC Vs Yanga SC

moodykabwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
625
Reaction score
602
Ngao ya Jamii ni taji ambalo huchezwa wiki moja kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Na: YANGA WHATSAPP SUPPORTERS MAKAO MAKUU.

Tunakukumbusha Kuelekea tu Tarehe 23/8/2017 Ngao ya jamii. Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii ni maalum kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi hiyo ya juu Tanzania Bara. Maarufu kwa jina la 'VPL'

Zamani ilichezwa baina ya bingwa mtetezi wa ligi na mshindi wa pili. Lakini siku hizi Bingwa wa Kombe la FA, ndiye anapambana na wa Ligi Kuu. Wakati tunasubiria mechi hiyo, yafuatayo ni matokeo ya mechi zote za Ngao ya Jamii tangu mwaka 2001.

1. Yanga 2-1 Simba (2001)
Hii ndiyo mechi ya kwanza ya Ngao ya Jamii, iliyochezwa Februari 17, 2001 baina ya watani hao wa jadi. Yanga ilifanikiwa kuchukua taji hilo na kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kufanya hivyo, kwa kuwafunga Simba mabao 2-1. Simba ilianza kufunga bao Steven Mapunda 'Garincha, kabla ya Edibilly Lunyamila alisawazisha dakika nne baadaye na Ally Yusuph ‘Tigana’ alipachika bao la pili dakika ya 80.

2. Mtibwa 1-0 Yanga (2009)
Timu ya Mtibwa Sugar iliingia kwenye rekodi ya kuwa moja ya klabu zilizotwaa Ngao ya Jamii 2009 baada ya kuifunga Yanga bao 1-0. Mechi hii ilichezwa baada ya miaka minane kupita, kwani tangu 2001 haikuchezwa tena.

3. Yanga 3-1 Simba-penalti (2010)
Yanga ilifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii, Agosti 18, 2010, baada ya kuwafunga mahasimu wao wa jadi kwa mabao 3-1, yaliyopatikana kwa kupigiana penalti baada ya dakika 90 bila kufungana. Penalti za Yanga zilifungwa na Geofrey Bonny, Stephano Mwasika na Isack Boakye. Penalti pekee iliyofungwa na Simba ilifungwa na Mohamed Banka. Okwi, Uhuru Selemani na Juma Nyosso walikosa.

4. Simba 2-0 Yanga (2011)
Simba ilifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza Agosti 17, 2011 ilipowachapa watani zao wa jadi Yanga. Haruna Moshi ‘Boban’ alifunga bao la kwanza, kabla ya Mzambia, Felix Sunzu kuongeza lingine kwa mkwaju wa penalti.

5. Simba 3-2 Azam (2012)
Septemba 11, 2012 Simba ilitetea taji lake la Ngao ya Jamii ilipoifunga Azam FC mabao 3-2. John Bocco alianza kuifungia Azam bao, kabla ya Kipre Tchetche kupachika la pili.
Dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza, Daniel Akuffor alifunga bao la kwanza, kabla ya Emmanuel Okwi kupachika bao la pili. Dakika nane baadaye, Mwinyi Kazimoto alipachika bao la tatu.

6. Yanga 1-0 Azam (2013)
Katika mechi hiyo, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa dakika ya pili tu ya mchezo na Salum Telela na kudumu dakika tisini.

7. Yanga 3-0 Azam (2014)
Yanga ilikutana tena na Azam kwa mara ya pili mfululizo mwaka 2014 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii. Katika mechi hiyo iliyochezwa Septemba 14, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na Geilson Santos na Simon Msuva.

8. Yanga 8-7 Azam - penalti (2015)
Golikipa wa Yanga Ally Mustapha ‘Barthez’ aliibuka shujaa kwa kupangua penalti mbili, akiiwezesha Yanga kutwaa Ngao ya Jamii Agosti 22, 2015. Katika mechi hiyo, Yanga iliifunga Azam FC kwa mabao 8-7 yaliyopatika kwa mikwaju ya penalti, baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana, ikiifanya kutwaa mara ya tatu mfululizo.

Barthez, alipangua penalti za Serge Wawa na Ame Ally ‘Zungu’, huku mwenzake Aishi Manula wa Azam akipangua moja ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’. Penalti za Yanga SC zilifungwa na Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amissi Tambwe, Andrey Coutinho, Godfrey Mwashiuya, Thabani Kamusoko, Mbuyu Twite na Kelvin Yondani. Penalti za Azam zilifungwa na Kipre Tchetche, John Bocco, Himid Mao Mkami, Aggrey Morris, Jean Baptiste Mugiraneza, Erasto Nyoni na Shomary Kapombe. 08 AUG 2016

Utaendelea Msimu uliofwatia usikose kutufwatilia

Imeandaliwa na

YANGA WHATSAPP SUPPORTERS MAKAO MAKUU
fbeb03fc0f525c9aff3fcdd96b0e2074.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viva Yanga.... Daima mbele, Nyuma Mwiko

Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
Pamoja na simu yako ya iPhone,
Yanga lazima wachapwe na Simba kwenye ngao ya jamii siku hiyo.
Kumbuka kwenye mtani jembe mmechapwa hadi mmeikimbia kabisa.
Ujue kichuya atakuwepo na Okwi na Boko na Asamoh na Niyoniyo
Ha..ha...ha... Ni kichapo tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manjiiiiiiii oyeeeeeeeeeeee

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Viva Yanga.... Daima mbele, Nyuma Mwiko

Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
Nilisikia simba wamegoma kuchukua medali za ushindi wa pili .....vipi ktk huu mchezo wa ngao ya hisani watashiriki vipi....kama vipi wawaachie kagera tucheze nao tu[emoji126] [emoji126] [emoji126] [emoji126] [emoji126] [emoji126]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NATAFUTA MTU WA KUWEKA NAE MZIGO... SIMBA 2 YANGA 1
 
Back
Top Bottom