Kuelekea nusu fainali Mayanga Zambia sio South jipange kikamilifu tuwaondoshe ila badilika

Kuelekea nusu fainali Mayanga Zambia sio South jipange kikamilifu tuwaondoshe ila badilika

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Taifa stars vs south Africa ,vilaza wawili wa soka wanaminyana hapo baadae ,

Siku kadhaa nyuma nilisema kwenye post yangu kuhusiana na mpambano wa Stars na South kuwa vilaza wawili wanakutana hivyo kubashiri mchezo huo ungekuwa vigumu haswa watu wa betting wawe makini sana bahati nzuri Stars ilifanikiwa kuwafunga Bafanabafana vilaza wenzetu kwenye mchezo wa soka.

Stars tumefanikiwa kuvuka na tunakutana na Zambia katika hatua ya nusu fainali ila tuseme ukweli Zambia wapo vizuri sana kuanzia ngazi ya klabu wanafanya vizuri timu kama Zesco,Zanaco nk wanafanya vizuri mashindano ya Africa na kwenye ngazi ya taifa Zambia hivi karibuni imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mipango mizuri ya chama cha soka cha zambia chini ya aliyekuwa kalusha bwalya. ni miaka michache tu Zambia walifanikiwa kubeba kombe la Afcon na hawakubeba kwa kubahatisha Bali mipango ya kalusha Bwalya ndio imewafanya Zambia wawe wazuri na tishio kwa namna moja au nyingine.

Nyota kama kapumbu,sinkala ,sunzu,kalaba wanafanya vizuri sana achana na akina chirwa waliosajiliwa 200M yanga kwa kuonekana bora lakini harufu ya national team haijui ,achana na mkata umeme wa yanga kuna akina kalaba ,sinkala,Kabwe .

Kwako Salum Mayanga Taifa stars imekuwa ikicheza kwa kujilinda sana kiufupi kupaki basi na mipira mingi inapotea kwenye sehemu ya kiungo nakutahadharisha hawa akina Sinkala,Kabwe ,kalaba sio watu wa mchezo mchezo badilisha uchezaji wa timu la sivyo tutaambulia dhahma kutoka kwa wazambia.

Tukiwafunga zambia basi 100% sina chembe ya shaka Stars watabeba cosafa ila kwasasa tujifunge mkanda kuwaondosha hawa ila Mayanga akiendelea na appeoach yake bora nisiendelee kusema.
 
Kila la heri Taifa Stars hapo kesho itakapotupa karata yake
 
Tunatofautiana unategemea wote tungekuwa tunaanzisha thread ingekuwaje wengine tupo kwa ajili ya kucoment
Kweli mkuu wengine wamejiwekea ratiba, kudrop thread mara 1 kwa mwezi au hata mara 1 kw mwaka na pale anapokuwa na jambo msingi..
So is decisions for someone
 
malinzi kawekwa lock up siku tatu tu tumefika nusu fainali...je akifungwa miaka mitatu? si tutaenda world cup fainali kabisa!! natania tu..

kikubwa Mayanga ajipange vyema Na pia awaweke sawa wachezaji kisaikolojia pia nashauri mtu kama Stamili Mbonde aanze maana Anauwezo wa kutumia nguvu kushambulia,

vile vile Banda kama yuko Ok anaweza kuanza,
 
Zambia B tunawafunga..
Wachezaji wa Ulaya plus Zesco na Zanaco hawatakuwepo
 
malinzi kawekwa lock up siku tatu tu tumefika nusu fainali...je akifungwa miaka mitatu? si tutaenda world cup fainali kabisa!! natania tu..

kikubwa Mayanga ajipange vyema Na pia awaweke sawa wachezaji kisaikolojia pia nashauri mtu kama Stamili Mbonde aanze maana Anauwezo wa kutumia nguvu kushambulia,

vile vile Banda kama yuko Ok anaweza kuanza,
Banda kazingua leo pamoja na mbonde
 
Kweli mkuu wengine wamejiwekea ratiba, kudrop thread mara 1 kwa mwezi au hata mara 1 kw mwaka na pale anapokuwa na jambo msingi..
So is decisions for someone
Ndio na hii inaondoa ile hali ya kulike na kucoment thread yako mwenyewe coz wote tutakuwa tumepost
 
Back
Top Bottom