Owen chimela
Member
- Feb 24, 2012
- 93
- 230
Ni Kama tumekubali matokeo ya October 2020
Kuna dhana ya muda mrefu ya kwamba kimya kingi kimebeba mengi..Kimya kingi kinaweza kua kimebeba uoga,ujasiri,usiri,unyonge au hata umakini hafifu was kuishi kesho Kama leo.
COVID 19 Imetutoa kwenye mstari halisi wa tafakari nzito juu ya siasa na maendeleo ya uchumi wa nchi yet kuelekea miaka mingi inayo..
Tumesahau yote yaliyofanyika kwa kipindi Cha miaka 4 iliyopita kwa Sababu ya janga la COVID 19...
Zipo dhana nyingi zinazoweza kujitokeza kuzungumzia mustakabali wa siasa kwa mwaka huu
Mosi : mwenendo wa siasa za mageuzi ya uchumi wa taifa na watu kwa miaka minne iliopita
Pili: Madai hai ya haki za binadamu na utawala Bora
Tatu: Nidhamu na utii ya viongozi kwa taifa letu
Mosi; Kuhusu mwenendo wa siasa shahidi zipo wazi kua hakukua na namna yoyote Ile ya uwazi Kati uwajibikaji wa vyama vingi vya siasa katika kutoa elimu inayotakiwa kwa umma ili kueleza uhusiano chanya unaoweza kujengwa Kati ya siasa na uchumi...Pengine Chama tawala (CCM) Kulingana na kwamba ndio pekee kilichopata muda wa kutosha kuzunguka nchi nzima kingejaribu kuelimisha Umma kuhusu siasa na mageuzi ya uchumi lakini kwa bahati mbaya kiligeuka na kuishia kupongeza juhudi za serikali ya awamu ya Tano pasipo kutoa maoni na muongozo unatakiwa kwa viongozi wakiotokana na Chama hicho.
Kuvilaumu vyama vya upinzani kwa kutokutoa elimu ya siasa ni Kama kuvionea kutokana na mazingira ya siasa yaliojengwa na serikali ya awamu ya Tano.Vyama vya upinzani vinatakiwa kulaumiwa kwa kukosa mbinu za ziada au mbadala za kutoa elimu kwa umma. Pia vyama vya upinzani vinatakiwa kulaumiwa kwa kukosa njia za ziada za kuweza kupambana na CCM ya kizazi hiki.
Pili, Madai ya haki za binadamu na utawala Bora yamekumbana na vikwazo ambavyo vinahimilika kikatiba na kisheria lakini kutokana na katiba hio hio wengi wameshindwa kupata Haki zao za msingi kwa wakati.Yote hio ni kwa sababu ya mazingira mabovu yaliotengeza muingiliano usiotakiwa wa mihimili mitatu ya serikali.Ni sehemu hio ambayo serikali imeishia kunyooshewa vidole na Kila mpenda haki kwa watu wengi kukumbwa na unyang'anyi wa haki zao za msingi. Katika hili serikali haitaweza kukwepa lawama kwani serikali ni sehemu ya watu wachache iliopewa mamlaka ya kuwawakilisha wengi.
Tatu,Nidhamu na utii wa viongozi kwa taifa..Hapa hakuna mwanasiasa alieweza kuuruka huu mtego . Ukiwasikiliza CCM walipokua wakizunguka baadhi ya pembe za nchi kuzungumzia namna Nchi bila CCM isivyowezekana,Wameuaminisha Umma hakuna Chama Bora kinachoweza kulitoa Taifa Hapa lilipo Kama CCM. Ukiwauliza ni Nani alielifikisha taifa letu Hapa lilipo leo hutaweza kupata jibu la kueleweka.
Vyama vya upinzani navyo havijaukwepa huu mtego ...Pamoja na kupata Airtime chache lakini wamejitahidi kutoa madhaifu ya Chama tawala kwa kiasi chake. Shida inakuja vyama hivi vinashindwa kutoa maoni ni kwa namna gani wao wangeweza kulitoa Taifa Hapa lilipo na kulipeleka mbele zaidi..Viongozi wengi wamekua watiifu wakubwa kwa vyama vyao pasi na kua na utii kwa taifa. Hakuna Chama kinachotoa a way forward kwa taifa zaidi zaidi Kila chama kinatoa a way forward kwa maslahi yake.
Tumejisahau kuelekea October 2020 lakini Kuna sauti inaniambia Tumekubali matokeo ya miaka minne iliopita...
Inahitaji uvumilivu mkubwa kupaka chumvi na asali kwenye kidonda cha kujikwaa kwa bahati mbaya.
Tanzania ilikuepo hata kabla siasa hazijabuniwa duniani na itakuepo hata pale ustaarabu wa dunia utakapobadilika
Tujikinge na CORONA