Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Ni wazi kuwa kama nchi hapa tulipo tukielekea Oct. 28 hatuko vizuri. Kwamba tunawagombea ambao wamejizatiti vilivyo kutokukubali kushindwa? Hili si jambo la afya hata kidogo.
Kwamba kuna mazingira ya kuwekeana vikwazo labda kutumia hata tume ya uchaguzi kuengua baadhi ya wagombea mezani kabla ya kufika kwa wananchi kuliko na nguvu ya sanduku la kura? Hili nalo si la afya kidogo.
Kwamba kuna mikakati labda ya kutumia hata mahakama kwa mgongo wa uhuru wake na au labda eti kufuata mkondo wa sheria? Hili nalo wala si la afya tena.
Kwamba pamejitokeza matumizi ya nguvu dhidi ya watu walioko katika shamrashamra zao zisizokuwa na athari na mtu yeyote kutoka kwa wengine au mamlaka? Ni wazi kuwa kama nchi tunaelekea kubaya.
Katika hali ya dharura sana, haya ni mambo ya kulaaniwa vilivyo na kila mpenda haki na mwenye kuipenda nchi hii. Mfano dhahiri wa ya kulaaniwa ni haya ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Arusha, Hai, Ruangwa nk na hata Mbeya. Wasiotutakia mema wanapaswa kufahamishwa bayana hivyo.
Mazingira wanayotaka kuyajenga kuwa hawatakuwa tayari kukubali kushindwa ni mambo ya kukemewa sasa kabla hatujachelewa kabisa.
Tunakwenda kwenye uchaguzi tukiwa na watia nia walio huru na sawa. Hakuna aliye na haki zaidi kuliko mwingine. Hakuna aliye mtanzania zaidi kuliko mwingine wala mwenye uzalendo zaidi kuliko mwingine. Uchaguzi si ugomvi.
Hatunaye leo Mzee Nyerere (rip). Hayupo Mzee Mkapa (rip). Busara zao zilihitajika mno sasa labda kuliko wakati mwingine wowote.
Mungu si Athumani mpo Mzee Kikwette na Mzee Mwinyi. Ni muda muafaka sasa labda zaidi sana kwa mzee Kikwette kutokulinyima taifa hili hazina ya busara zake.
Ni muhimu sana kwa Mzee Kikwette katika hali ya sasa akahusishwa moja kwa moja katika kuweka mazingira mazuri ya kufahamiana. Mustakabala na ujenzi wa salama katika nchi yetu hauwezi kuwa mikononi mwa "wawamba ngozi au ngoma" peke yao.
Uchaguzi si uadui. Uongozi ni wa Watanzania si wa mtu binafsi wala chama binafsi.
Yasemekana tayari tumekwisha poteza mtu mmoja. Hebu na asipotee wala kuumizwa mwingine kwa sababu ya uchaguzi tu.
Matumizi yoyote ya nguvu, janja janja, laghai, hila, husuda na vyote vya namna hiyo tokea kokote visipewe nafasi.
Polisi, mahakama, tume ya uchaguzi na msajili wa vyama vya siasa wajikite kwenye majukumu yao yaliyo ya msingi zaidi. Hebu wasiwabughudhi au kutumika kuwabugudhi wanasiasa au watia nia. Tuipe nafasi busara kutawala kuliko mabavu.
Hatukujifunza bado tokea katika matukio mengi mema tu yaliyo kwenda kinyume na matakwa ya maadui zetu?
Muda wa kuiponya nchi yetu ni sasa
Tulipo tunahitaji busara zaidi kuliko vinginevyo. Kwa kiswahili fasaha tuseme, "anahitajika zaidi sasa mwenye kuweza kumfunga paka kengele."
Wito: Huu ni muda muafaka wa maongezi. Kumhusisha rais mstaafu Mzee Kikwette sasa, angalipo lingekuwa jambo la heri sana.
Busara za mzee huyu zisizokuwa na upendeleo wowote zisikilizwe na pande zote. Tanzania ni kuu mno kuliko mtu au chama chochote:
Wito: Chonde chonde, Tanzania ni zaidi mno ya yeyote
Nawasilisha.