Kuelekea Pambano la Simba na Yanga 26.9.2015, Ukimya wa Yanga Unanitisha

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Posts
1,544
Reaction score
943
Imezoeleka kila inapokaribia mechi ya Simba na Yanga kumekuwa na tambwee nyingi, kejeli na kimuhemuhe cha kila namna kutoka kila upande. Na kwa mtazamo wa wapenzi wengi wa Simbaa, Yanga inajulikana kama ''noisy neighbours'' kwa maana kuwa wanachonga sana naa ndio maana inaitwa timu ya magazetini. Mfano mechi iliyopita Mzee Akilimali alicheka kicheko cha dharau sana kabla ya mechi na kutamba kuwa ilikuwa lazima Simba apigwe 3-0!
Baada ya Yanga kuangukia pua baadhi ya vyombo vya habari vikawa vinatumia kicheko kile ktkk vipindi vya michezo ili kunogeshaa mambo.

Lkn kuelekea mechi hii ya Jumamosi kuna ukimya unaotisha na usiozoeleka hasa kutoka upande wa Yangaa. Je hii inatokana na nini? Ni hofu, heshima kwa mtani, tahadharii au wamejifunza kutokana naa makosa na hivyo kuamua kukimbiza mwizi kimyakimya?
 
kuwe na ukimya au kelele mikia lazima iliwe tu hakuna namna
 
Mnataka tupige kelele kwani kuna wasiosikia au kujua mnyama analiwa akiwa m'bichi iyo jumamosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…