Kuelekea Siku ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya kama nchi tujitathmini

Kuelekea Siku ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya kama nchi tujitathmini

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Tunapo elekea kwenye kilele cha maadhimisho ya kimataifa ya kupambana na madawa ya kulevya ambapo kilele ni tarehe 1/7 na trh. 2/7, kama nchi tunapaswa tujitathimini hali yetu kama nchi, Je vita ya kupambana na madawa ya kulevya insaidia kupunguza au hali ni mbaya?

Nini kifanyike ili kukomesha madawa ya kulevya.

Wauza madawa ya kulevya tunaishi nao ktk mitaa yetu, tuwafichue.

Tunaziomba mamlaka za kupambana na madawa ya kulevya wasirudi nyuma wala wasiwaonee aibu wauza madawa ya kulevya.

Tupambane na dawa za kulevya kwa vitendo sio maneno. wananchi wanataka kuona wauzaji wanakamatwa na kufungwa jela.
 
Solution NI makonda only..hakuna kiongozi aliyewahi kutokea kuwa na Nia ya dhati ya kupambana na madawa zaidi ya makonda na boss magufuli
 
Solution NI makonda only..hakuna kiongozi aliyewahi kutokea kuwa na Nia ya dhati ya kupambana na madawa zaidi ya makonda na boss magufuli

Nakubaliana nawe kuwa aliye kuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM ndg. Makonda alijitoa muhanga ktk kupambana na wauza madawa ya kulevya bila woga hakika hivyo ndivyo kiongozi anatakiwa awe, hakuna sababu ya viongozi wetu kuwa waoga kwenye vita hii, kama huweza kaa pembeni, maana vita ya kupambana na madwa ya kulevya sio lelemama inahitaji watu walio dhamiria kuwatumikia wananchi sio kulinda "kitumbua".

Viongozi tuache tabia ya kuhangaika na mambo madogomadogo tuakaacha mambo serious kama haya ya kupambana na wauza madawa ya kulevya.

cheo ni dhamana, timiza wajibu wako.

Kiongozi huwezi kupendwa na watu wote, wala tusitake kupendwa bali tunapaswa kufanya kazi kwa manufaa ya nchi na wananchi.
 
Tuanze kuwafichua wauza madawa ya kulevya ambao wapo kwenye maeneo yetu mfano; sinza, kinondoni, Temwke, mbezi, bunju, tegeta, k.koo, n.k, n.k. Tutoe taarifa za siri ili wakamatwe
 
Ila inabidi napo kuwe na siku ya kupambana na Pombe. Maana nayo inamaliza vijana mitaani huku na tunaichukulia poaa tu
 
Toa taarifa ya siri kupitia namba ifuatayo;

119

Tuwafichue wauza madawa ya kulevya. Tuokoe jamii yetu dhidi ya athari za madawa ya kulevya.

Wauza "unga" tunaishi nao mitaani shime wananchi wenzangu tuwafichue, zawadi zipo.
 
Madawa ya kulevya ndio chanzo cha aina zote za uhalifu, kama vile ujmbazi n.k, hivyo kama tutapambana na madawa ya kulevya kwa nguvu zetu zote na kwa maarifa yetu yote hakika usalama na amani ya nchi yetu itaendelea kuwepo vinginevyo tutaumia.
 
Toa taarifa ya siri kupitia namba ifuatayo;

119

tuwafichue wauza madawa ya kulevya.
tuokoe jamii yetu dhidi ya athari za madawa ya kulevya.

Wauza "unga" tunaishi nao mitaani shime wananchi wenzangu tuwafichue, zawadi zipo.
Shida unatoa taarifa alafu hatuna uhakika na usalama wetu

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Shida unatoa taarifa alafu hatuna uhakika na usalama wetu

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
Usalama ni asilimia 100, wewe toa taarifa moja kwa moja kwa Kamishna, usipitie kwa viongozi wa eneo lako.
Usalama upo sana na pia zawadi zipo kwa mujibu wa maelezo ya kamishna, ilimradi tu taarifa ziwe za uhakika sio longolongo.
 
Tushirikiane kuwafichua wauza madawa ya kulevya wote.
 
Back
Top Bottom