Ni ukweli usiopingika kuwa CHADEMA ndicho chama kinachovuta hisia za Watanzania walio wengi bila shaka kuliko CCM na chama kingine chochote cha siasa na kwamba katika mazingira huru CHADEMA kinauwezo wa kushinda uchaguzi mkuu na kuwa chama tawala.
Kwanini CHADEMA pamoja na haya yote kinaishia kupata chini ya 1% ya kura mfano uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa inaonesha jinsi ambavyo watanzania tunapaswa kutumia njia za ziada kuondokana na mfumo CCM uliokwisha kujichimbia kwa kutumia dola na kufanya watakavyo bila kuchukuliwa hatu yoyote.
Mbowe vs Lissu
Mbowe ndio amekifanya CHADEMA kuwa hapo kilipo sasa; chama kikuu cha upinzani chenye mvuto na ushawishi mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea nchini.
Lissu ni mwanasiasa mwenye mafungamano makubwa na uanaharakati wa muda mrefu na uliopo kwenye hulka yake ya asili, mchango wake CHADEMA ni mkubwa pia hasa siku za karibuni.
Mbowe ni mwanasiasa mwenye diplomasia na hupendelea zaidi kutatua migogoro ya kisiasa kwa njia ya mazungumzo na makubaliano.
Lissu ni mwanasiasa wa kiharakati ambaye hupendelea zaidi kusimamia msimamo wake bila kukubaliana na hoja za upande wa pili katika kufikia muafaka wenye kuridhiwa na pande mbili.
Mbowe ana uzoefu mkubwa wa kuongoza CHAMA na ana ukomavu mkubwa wa kifikra akijua hali halisi na mapungufu ya demokrasia ya Tanzania na kwamba demokrasia iliyokomaa ni mchakato wa muda mrefu.
Lissu anaishi zaidi nadharia za kidemokrasia na angependelea kuona Tanzania inakuwa na demokrasia kama ile ya Marekani leo hii.
Mbowe anaungwa mkono zaidi na wanamapinduzi watulivu na wenye uvumilivu wa kisiasa.
Lissu anaungwa mkono zaidi na wanamapinduzi wa kiharakati na wasio na uvumilivu mkubwa kisiasa.
Mbowe anakwepa malumbano binafsi yenye lengo la kuepuka mpasuko ndani ya CHADEMA.
Lissu anapendelea zaidi malumbano binafsi (confrontation) yasiyojali suala la kuigawa CHADEMA.
Kama atakuwa mwenyekiti:
Mbowe ataendelea kuifanya CHADEMA kuwa chama chenye muonekano wa kidemokrasia ya mrengo wa kushoto (msimamo wa kawaida).
Lissu ataifanya CHADEMA kuonekana chama chenye mrengo wa kulia (msimamo mkali).
Mbowe ataendeleza mazungumzo ambayo baadaye yanaweza kuleta serikali ya umoja wa kitaifa kupitia mazungumzo.
Lissu anaweza kuleta serikali ya umoja wa kitaifa kupitia maandamano.
Mbowe ataendelea kuwa nguvu ya kuunganisha makundi mbalimbali ndani ya CHADEMA.
Lissu anaweza kuzidisha utengano ndani ya CHADEMA na kufanya mpasuko zaidi.
Mwisho:
Mbowe ana nafasi ya kufanya CHADEMA mpya kwa uzoefu wake na yote aliyojifunza hasa hivi karibuni.
Lissu ana nafasi ya kuleta mwamko mpya CHADEMA lakini pia kufanya makosa yatakayoigharimu CHADEMA.
CHADEMA wameonesha kuwa ndicho chama chenye kuvuta hisia za watanzania wengi zaidi na kwamba kama mazingira ya demokrasia na uchaguzi huru yatakuwepo ni dhahiri CHADEMA kitashinda uchaguzi mkuu na kuongoza nchi.