Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

mtingi1

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2020
Posts
957
Reaction score
935
Poleni kwa msiba wa Taifa, Mwenyezi Mungu atufariji sote kwa kuondokewa na Rais wetu mtaafu mzee Mkapa, RIP.

Niende kunako hoja yangu juu ya UCHAGUZI ujao, nionavyo mimi, uchaguzi huu unaweza kuwa na MVUTO like never before, tazama mapokezi ya Tundu yalivyokuwa, regardless ya msiba mzito, watu wamejitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi wao/mtanzania mwenzao.

Hii inaashiria nini? tusubiri tuone.

Mchakato wa kura za maoni pia kwa CCM umekuwa wa kipekee sana mwaka huu, hongera kwao.

Ili uchaguzi upendeze, niombe vyombo vya habari vyote, vitoe fair grounds kwa Vyama vya Siasa, wasiwe na upendeleo kwa chama chochote.

Ni wazi CCM itashinda but kukiwa na uwanja sawa wa kiushindani, CCM kitapata ushindani mkali sana pengine kuliko hata wakati wa mzee Lowassa.

Ni mawazo yangu tu lakini, mimi mtanzania nisiye na chama chochote. Ningependa ipatikane idadi nzuri ya wabunge wa upinzani bungeni, ili bunge liwe na mvuto.

Niwatakie nyote maombolezo mema.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kikwazo kikubwa cha wapinzani hata wakiungana ni tume ya uchaguzi tuliyonayo kwa sasa. Tume siyo huru hata kidogo.
 
Back
Top Bottom