SoC02 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025: Tume huru ni muhimu kuliko Katiba mpya?. (Katika mtazamo wangu)

SoC02 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025: Tume huru ni muhimu kuliko Katiba mpya?. (Katika mtazamo wangu)

Stories of Change - 2022 Competition

samwely1

Member
Joined
Jan 2, 2014
Posts
12
Reaction score
3
Utawala bora unajengwa kwa kuwa na katiba imara na madhubuti, inayoendana na wakati. Katiba yetu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ni miongoni mwa katiba kongwe ambayo pasi na shaka yako mambo kadha wa kadha yanayohitaji mabadiliko ya haraka sana. Hili linajidhihirisha kupitia mapendekezo yaliyokusanywa na tume ya mabadiliko ya katiba yalizaa rasimu ya katiba pendekezwa mapema mwaka 2014. Miongoni mwa mengi yaliyopendekezwa lipo swala la Tume huru ya uchaguzi. Kuzingatia muktadha huo hapa tutaangazia swala la Tume huru ya uchaguzi.

Kabla ya kufika mbali na tujiulize, ni kipi muhimu kuanza nacho kati ya Katiba mpya ama Tume huru ya uchaguzi? Ni dhahiri msukumo wa kupata ufumbuzi wa mambo haya mawili unatokana na yaliyotokea katika uchaguzi wa serikali za mtaa 2019 pamoja na uchaguzi mkuu 2020. Chaguzi ambazo zililalamikiwa kughubikwa na kiwango kikubwa cha uonevu kwa vyama vya upinzani hali iliyopelekea kushuka kwa idadi ya wabunge kutoka vyama pinzani. Kwa mfano kutoka uchaguzi mkuu 2020 ni wabunge wa nne tu kutoka vyama pinzani ndio walichaguliwa, idadi ndogo kabisa kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya miaka 15 nyuma. Sababu hii pamoja na sababu nyingine lukuki ndizo zinazotoa msukumo mkubwa wa kuhitaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Nini Kianze (Katiba ama Tume Huru ya Uchaguzi)

Yote mawili yana umuhimu mkubwa, na ni dhahiri katiba ndio huzaa Tume ya uchaguzi, lakini kwa kuzingatia muda na wakati kuelekea 2025 hatuna budi kufanya machaguzi ya nini kifanyiwe kazi mapema zaidi kati ya hivyo viwili. Leo ni 2022, ni miaka miwili kuelekea 2024 amabapo tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mtaa, na ni miaka 3 kuelekea 2025 ambapo tutakuwa na uchaguzi mkuu. Kwa muktadha huo, ni dhahiri kupata katiba mpya katika kipindi kilicho salia kuelekea 2025 ni jambo gumu, kwani hakuna asiyejua kuwa ili kupata katiba imara inahitajika mchakato shirikishi ambao swala la muda haliepukiki.

Katika kutambua hilo kama wakati wa mpito, ni bora kukawa na maridhiano ya pamoja baina ya serikari, vyama vya siasa pamoja na wadau kukubaliana kufanya maboresho ya muundo ya wa sasa wa Tume ya uchaguzi kwa kuzingatia maoni yale yaliyomo kwenye rasimu ya mabadiliko ya katiba ambayo tayari wanachi waliyawasilisha na yakachambuliwa na tume ya mabadiliko ya katiba iliyooongozwa na Jaji Warioba. Hii inaweza kuwa ni njia nzuri kupata muundo mzuri wa tume huru ya uchaguzi kama ambavyo kilio cha vyama vya siasa hasa upinzani unavyohitaji kuelekea 2025. Maoni yale kwenye rasimu ni maoni ya wananchi hivyo katika kipindi hiki cha mpito kabla ya katiba mpya yaweza tumika katika kufanya marekebisho ya kimuundo ili tume iwe huru na ikatende haki katika uchaguzi 2025.

Nini kiboreshwe kupata tume huru ya uchaguzi katika kipindi hiki tukisubiri kufufuliwa kwa mchakato wa katiba mpya.

Moja; kwakuwa ipo sheria inayosimamia uchaguzi, basi kupitia sheria hiyo kiuundwe chombo maalumu ambacho ndicho kitakuwa kamati maalumu ya uteuzi wa viongozi wakuu watakaosimamia uchaguzi. Chombo hiki kihusike moja kwa moja katika uteuzi wa mwenyekiti wa tume, makaamo mwenyekiti, na wajumbe. Hii ina maana kuwa, madaraka ya uteuzi ambayo yalikuwa yanashikiliwa na Raisi yatakuwa yamegatuliwa ili kupunguza ukakasi wa imani juu ya wateuliwa ambao kama watateuliwa na Raisi huwa ni kutoka upande wa chama chake.

Pili; pamoja na kuwa na chombo amabacho ndicho kitakachokuwa na uhalali wa kuwateua viongozi wakuu wa tume ya uchaguzi, lakini ipo haja uteuzi huu ufanywe baada ya kutangaza wenye kukidhi sifa na vigezo katika nyazifa hizo kutuma maombi. Hivyo chombo hichi kitateua Mwenyekiti, makamo, mkurugenzi wa uchaguzi pamoja wajumbe kutika katika maombi yaliyoombwa na wanaoona wana sifa kuhudumu katika nafasi husika. Hii itasaidia kuteua watu wenye sifa na waadilifu.

Tatu; Ni lazima kuwepo na mazingatio ya usawa wa kijisia pamoja na uwakilishi sawia kutoka pande zote mbili za muungaao katika teuzi. Hii ina maana kuwa lazima kuwe na 50 kwa 50 kubalansi usawa. Lakini pia ili tume hii iwe huru na haki ni lazima endapo mwenyekiti atatoka bara basi makamo mwenyekiti atoke upande wa muungano, hivyo hivyo kwa wajumbe na mkurugenzi wa uchaguzi.

Hitimisho
Kama muundo huu utatumika katika kuunda tume huru ya mpito ni dhahiri itapunguza malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitajwa na vyaama vya siasa hasa vyama vya upinzani. Kwa kuwa uteuzi wa viongozi wa tume utazingatia mchakato wa wazi kupitia maombi basi hii si tu itazuia kuteua mamluki wa vyama bali pia itasaidia kupata watu weledi, wenye uzoofu pamoja kuwafanya wafanye kazi pasi na kuingiliwa ama kupata maelekezo kutoka upande wowote.

Pamoja na hayo, uko ulazima wa kufanya mabadiliko ya nani katika ngazi ya majimbo atakuwa ndiye mtangazaji wa matokeo ya uchaguzi kwa ngazi ya ubunge na udiwani. Hivi sasa wakurugenzi wa wilaya ndiwo wenye mamlaka ya kumtangaza mshindi katika ngazi ya ubunge na udiwani, jambo hili nalo bado lina ukakasi kwani wakurugenzi wote ni wateuliwa wa raisi ambao kimsingi ni makada wa chama tawala hivyo wao kubakia kuwa ndiwo watangaza matokeo katika ngazi ya jimbo bado hakutoi taswira nzuri kwani vyama vingine inawawia vigumu kuwa na imanai nao kwakuwa wapo pale kutekeleza matakwa kutoka katika mamlaka zao za uteuzi. Hivyo ili maboresho haya yawe na mashiki iko sababu na wao wapokwe madaraka hayo ili kutoa uhalali zaidi wa matokeo yanapotangazwa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom