WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 456
Huko nyuma niliwahi kuandika ujio wa Bernard Membe ndani ya ACT na hatma ya coalition au ushirikiano wa vyama vya Siasa. Nilieleza kwamba Membe ameingia ACT-Wazalendo akiwa tayari na uamuzi wa kugombea urais mfukoni huku akivitaka vyama vingine vya upinzani vimuunge mkono. Kwake yeye haamini uwepo wa wagombea wengine wenye nguvu katika vyama hivyo. Anaona ni yeye pekee mwenye turufu.
Nilijaribu pia kupima nguvu ya Membe. Kwamba ujio wake ndani ya upinzani una faida gani? Nilimweka katika mizania na Edward Lowasa. Nikahitimisha kwamba Membe ana faida ndogo. Kwanza ni katika mtaji wa watu ambapo hadi sasa hatusikii akiungwa mkono kwa uwazi na makada wenye nguvu ndani ya CCM. Katika hili Membe ameingia ACT-Wazalendo akiwa yatima bila kuwa na mtaji wa watu. Anategemea mizizi ya chama hicho kichanga badala ya yeye kutegemewa zaidi. Pili; Kwa zaidi ya miaka mitano, Membe alipotea kabisa katika ulingo wa kisiasa na hata kwenye matukio jumuishi ya wanasiasa.
Ni ngumu kumpima nafasi yake nje ya CCM ingawa hata ndani ya CCM kwenyewe inaonekana alishapoteza mtandao aliokuwa ameujenga. Hili pamoja na historia waliyoiacha makada wa CCM chini ya Lowasa waliotimkia upinzani mwaka 2015 na baadaye kurudi nyumbani inakiweka ACT-Wazalendo na Membe katika wakati mgumu kisiasa hasa upande wa Tanzania Bara.
Katikati ya njia panda, vijana wa ACT-Wazalendo wakiongozwa na Zitto Kabwe na Ismail Jussa wameanza kutafuta kwa udi na uvumba ushirikiano wa vyama vya upinzani hususan CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu. Bahati mbaya hili wameliingia ‘mazima’ kitaasisi bila kujali wenzao wa CHADEMA wanaweka nguvu kiasi gani katika kulipigia chapuo. Tumeona wakivalia njuga suala la kuzuiliwa mahabusu ya Singida vijana wa CHADEMA akiwemo Katibu wa Baraza la Vijana Nusrat Hanje na wenzake kuliko hata CHADEMA yenyewe. Ingawa chama hiki kweli kimekuwa kikiisemea dhulma dhidi ya haki ni dhahiri kwa sasa kitendo cha Ngome ya Vijana-ACT kuamua kuitisha press conference juu ya suala hili lengo ni kujenga uzengezi na kutafuta njia ya public kushawishi ushirikiano wa vyama hivi. Bahati mbaya wazo hili halinunuliki kwa upana.
Hata hivyo, ACT-Wazalendo wanasahau kitu kimoja. Mwenendo na mfumo wa siasa anazozifanya Kiongozi wao Zitto Kabwe ni za kujijenga yeye zaidi kuliko kujenga daraja la huo ushirikiano. Mathalani, wakati akihojiwa na Jenerali Ulimwengu kupitia channeli yake ya YouTube ya Jenerali online, Zitto alionekana kukosoa ushirikiano wa vyama uliofanyika kupitia UKAWA mwaka 2015. Alienda mbali akidai CHADEMA haikuwa rafiki kwa makada wa CCM akiwemo Lowasa waliojiunga nacho. “Hakikuwafanya wajione nyumbani’. Hili alilisema huku akijinasibu kuwa yeye ni bingwa wa kubuni mazingira rafiki kwa makada wapya waliojiunga na chama chake. Mbaya zaidi vijana hawahawa wa ACT-Wazalendo walikuwa frontline ku amplify hiki.
Pili; wakati viongozi wa CHADEMA wanapigwa spana kuingia Uwanja wa Uhuru kuuaga mwili wa Rais wa awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa, hakukuwa na nguvu ya vijana hawa wa ACT-Wazalendo kukemea, badala yake walijikita katika kujenga siasa zogozi za kumpamba Maalim Seif Sharif Hamad aliyefanikiwa kuhudhuria tukio kama kiongozi mstaarabu, mwenye kujua itifaki na muungwana. Lengo lilikuwa kujenga taswira kwamba viongozi wa CHADEMA kukosekana ilikuwa mwendelezo wa siasa zao katika msiba huo.
Katika mazingira haya imani ya kuujenga ushirikiano inakuwa ngumu. Ingawa sifahamu behind the scene makubaliano haya ya vyama kuuelekea ushirikiano wao itoshe kusema kwamba mazingira haya tayari yanasimika mizizi ya kutokushirikiana. Katika kucement hoja hii Aliyekuwa Mbunge wa Kawe ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Halima James Mdee alijitokeza waziwazi na kumvaa mmoja wa vijana wa ACT-Wazalendo Sufian Juma aliyekuwa aki amplify kauli ya Zitto iliyokosoa mfumo wa CHADEMA kupokea na kuishi na waliokuwa makada wa CCM waliongozwa na Lowasa (Tazama kiambatanishi cha Picha) Kwa ufupi hali ilivyo naweza sema is too late kwa ACT-Wazalendo kuupata ushirika na CHADEMA.View attachment 1525770
View attachment 1525771