Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Nyie nanyi mmetuchosha kwa hoja zenu dhaifu, mmevaa miwani yenye vioo vya mbao kiasi kwamba ukweli hamuuoni? Safu ya uongozi Chadema ni familia ya nani? Njooni na hoja za msingi.

Tuje na hoja gani wewe?nyie ndo wa kuwachapa fimbo.
 
<<Haya ndiyo mambo tunayoyakataa na tunayoyapinga, woga na vitisho eti kwa sababu analindwa mwenyekiti asipingwe kwa sababu ya neno umoja wa chama, huo ni upuuzi na yeyeto aliye ukubali ni mpuuzi, na kama Zitto alitoa jina ili amwachie Mbowe free ride naye hajui analofanya kwani hio sio demokrasia, kwani hakuna demokrasia ya chumbani>>.

Kinepi,
Na huko kulindana ndiko ambako tumekupigiaga kelele majuzi hapa kwenye taarifa za mkutano wa NEC Dodoma. Sasa CHADEMA yetu takatifu inatupelekea huko tulikokupigia kelele. Inaelekea wanajaribu kutuambia "WE DON'T CARE, YOU CAN GO TO HELL!"

Kwa bahati muzuri madhara ya tabia kama hii katika chama ambacho bado hakijapata madaraka si makubwa sana lakini ole wetu, tumekwisha onywa! Swali la kutafakari ni kuwa tukiwapa madaraka CHADEMA nini kitawazui kuendelea kulindana na kutuletea RICHMOND, EPA, KIWIRA round 2 katika mtingo wa KULA KWA ZAMU? Kwanini tuendelee kuamini kuwa wao tukiwapa madaraka watabadirika?
 
ee mungu baba uwaangazie viongozi wote mwanga wa kutambua
kuwa yote wafanyayo ni kwa manufaa ya wanainchi na si kwa
maslahi yao binafsi.amen
 

Tatizo lako Moshi ni Uchaga na wala sio lazima uwe mwanachama wa chama cchochote.

Nimesoma baadhi ya michango yako linapokuja suala la Mbowe au CHADEMA ni kwamba uko biased kama lilivyo gazeti la Mtanzania Daima.

Ni ngumu sana kutengenisha Uchaga na CHADEMA na kumekuwa na tuhuma hizo tokea 2005 lakini hakuna juhudi kubwa iliyofanywa kuondoa tatizo hilo.

Watu ambao mnashinda hapa kutetea demokrasia sasa mnaaza kuja na sababu zisizo na msingi kuhalalisha hii rape juu ya demokrasia ambayo imefanywa na hao wazee wa CHADEMA.

Kwa mtindo huu msitegemee kupata majimbo huku kwetu kusini; endeleeni kubaki chama cha watu wa Kaskazini.

Mwaka huu tutawaambieni ukweli hata kama moderators kazi zao ni kufuta jumbe za wengine.
 
Mheshimiwa Zitto,lini utatoa official statement ili ukate mzizi wa fitna?
 
Wazee mimi nampongeza Zitto sana kwa kujitoa....Chadema ni chama kichanga sana ambacho kinahitaji kukubaliana kama taasisi kukijenga, si wakati wa kutofautiana hata kidogo tena linapokuja suala la kitaifa kama mwenyekiti wa chama. Haikuwa sawa kabisa kwa Zitto kuchukua form, alikosea na akatambua hilo ndo maana akajitoa. Yeye sio mpumbavu mpaka ajitoe tu kwa shinikizo, bali ametambua alipoenda pembeni na kuona bora akose yeye ili chama kisimame. Lazima tukubali Chadema kama chama kimepiga hatua chini ya uongozi wa Mbowe, na kazi walioifanya bado haijafikia tamati bali ule ushirikiano na uongozi unatakiwa upatiwe nguvu ya umoja ili matunda zaidi yaweze kufikiwa. Nimemheshimu sana Zitto kwa kujitoa, hajajiangalia yeye bali aliangalia chama zaidi. Chadema bado ni taasisi ndogo sana, you cant risk kuleta ufa hasa wa kifikra katika ngazi ya taifa halafu chama kikasimama, even in the name of democracy.....
 
Kwani lidhiwani kikwete na kiwete inakuwaje au umemuona Lucy peke yake. Makamba na mwanae pale ikulu vipi?


Mwambie pia Hawa Ghasia na Kikwete vipi?? Na IGP Said Mwema na Kikwete vipi? Tukiendelea kutaja list haitamalizika??!!! Ila kwa Chadema, wote waliochaguliwa ni wachapa kazi. Ni mambo mangapi mazuri Mzee Ndesamburo amefanyia Moshi ambayo kwa miaka takribani 48 ya Uhuru serikali haijaweza kufanyia wananchi wake??? Ni michango mingapi Bungeio Lucy na Baba yake wametoa katika Bunge letu?? Yule mzee huwa hasinzii Bungeni kama wale vilaza wengine wa ssm. Nampa big up kabisa. Na huyu mtoto wake ni hodari sana, she is strong na anafahamu anachokifanya.

Kuna member ameulizia eti hakukuwa na wapare katika wagombea?? Inawezekana walikuwepo, ila watawahakikishia vipi wananchi na wazalendo wa Moshi mjini kuwa wanaweza kufanya mambo ya maendeleo ya Moshi mjini kumshinda mzee wao Ndesamburo?? Ni vigumu just to take someone new on board kama hujaona matunda yake?? Ya mzee Ndesamburo na mwanaye yameshaonekana na hawana budi kuendelea kupatiwa nafasi zaidi ili waendelee kuwatumikia wananchi.
 
Acheni uzushi wenu huo maana kila wakati chadema sio chama cha kikabila. Wanafanya kazi nzuri sana
 
 

Watu kumbe bado mna fikra finyu namna hii....Chadema na uchaga wapi na wapi??????
 

Nafikiri hiz ni propaganda.
 
Kumeanza kunuka uchagga sawa na ukikuyu kwa wale wenzetu
 
Hii ndiyo Kamati Kuu ya CCM:
1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe23.Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe30 . Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe31 . Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe32 . Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe34 . Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe37 . Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe38. Ndugu Yussuf Moh’d Yussuf - Mjumbe
 
Niliwahi kuambiwa na Mzee mmoja kuwa yapo MAKABILA ambayo yana MSIMAMO usioyumba hasa wakishafanya UAMUZI ambao ni SAHIHI. WAHA sio moja ya makabila haya. Kwa kweli alinipa sifa mojawapo ya makabila haya ni kwenda jandoni kufanyiwa tohara wanaume kwa wanawake. Nitaonekana mkabila kwa baadhi yenu na pengine mtadhani nadharau baadhi ya makabila nchi hii.
Naongea haya kwa HASIRA sana. Naamini angekuwa MBOWE kwenye nafasi ya ZITTO asingeondoa jina!
 

wewe wasema,kwani chacha aling'ang'ania na mwisho wake ulikua upi?
 
Mkuu japo nimechelewa kuchangia mada na inawezekana baadhi ya mambo yameisha fanyiwa maamuzi lakini wacha niweka mawazo yangu kidogo.

Mimi nijuavyo Demokrasia inapokuja issue ya kuchagua ni kuwa kila mmoja ana haki ya kuchaguliwa sidhani kama umri ni kikwazo. Lakini inabidi tujiulize je kweli ZITTO KABWE ameiva vya kutosha kuweza kuongoza taasisi inayokua kama CHADEMA?

Watu wamechangia mengi ya kuponda lakini tujiulize kama kweli ZITTO alikuwa na nia ya dhati mbona hata viongozi wake wamemshangaa? Maana mtu unapokuwa unataka kufanya kitu kizito kama hicho lazima uombe ushauri ili kama kuna tatizo liweze kuwekwa sawa. ZITTO BADO ANATAKIWA KUANDALIWA ILI AWEZE KUWA MWENYEKITI MZURI atakaye kipeleka chama kinakotakiwa kwenda. Lakini kwa sasa jamaa bado mbichi sana. Ametumia tu umaarufu wake sidhani kama alikuwa amedhamilia kiukweli kugombea. WAPAMBE NDIYO WAMEMSHINIKIZA.

KAMA ZITTO KWELI AMEAMUA MWENYEWE BILA KUSUKUMWA NA WATU FULANI ASITOE JINA LAKINI KAMA KUTUMWA KUFANYA HIVYO AFANYE HIVYO AONDOE JINA LAKE.

SIASA ZA BONGO ZIMECHAFUKA HIVYO INABIDI TUANGALIE MAMBO KWA MAPANA YAKE SIYO KURUKIA VITU KWA JUU TU.

Labda kwa kuweka jina alitaka kutumia turufu kama ya kikwete 1995 lakini vinginevyo bado jamaa ni kijana mdogo anatakiwa kupikwa ili aweze kuwa kiongozi shupavu zaidi na mwenye maamuzi ya busara. Siyo ya kukurupuka kama alivyofanya.

Pia kuna ukweli mwingine kuwa CHADEMA wanamtegemea sana MBOWE kwenye mambo yao (sidhani kama kuna makubaliano kuwa mpaka awe mwenyekiti) na pia CCM wanamgwaya jamaa kwani irrespective ya mashambulizi yote wameshindwa kumjeruhi na much less CHADEMA yenyewe. Hivyo ZITTO kujiingiza kichwa kichwa kawapa jamaa turufu kwani SIASA za vyama sasa ni very delicate. Uamuzi wowote unaweza kuleta balaa kama ilivyotokea. Sidhani kama CHADEMA wangekuwa na nia mbaya ya kutowapa VIJANA nafasi hao wote wanaowika sasa tungewajua ikiwemo na ZITTO mwenyewe. Lakini kwa nafasi sensitive kama hizi lazima jamani watu waandaliwe vizuri.

Mimi sisupport ZITTO kuwa mwenyekiti kwa sasa bado ajapevuka vya kutosha. Anaitaji miaka kama mitano zaidi kukaa sawa. Kama ambavyo imevumishwa kuwa no. 1 wanawasiliana naye sasa maamuzi kama haya lazima yaangaliwe vizuri.
 
wewe wasema,kwani chacha aling'ang'ania na mwisho wake ulikua upi?
Tukiendelea na WOGA huu, CCM itatawala kwa KARNE nyingi zijazo! Tulimjadili sana Chacha, tumwache apumzike tu huko aliko kama kweli kuna maisha mengine baada ya kifo.
 


Kwahiyo unataka kutuambia kwasababu ya uchanga wa vyama vya upinzani CCM waendelee kuongoza?au una maana gani wewe.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…