mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Bunge limekwisha kuvunjwa, uwanja wa kisiasa sasa uko wazi ukisubiri wagombea watinge na kuanza kushindana.
Miaka 5 ya utawala wa CCM na Serikali yake, chini ya Rais Magufuli, nayo inafika ukingoni.
Siasa ndani ya hiyo miaka mitano imeghubikwa na mashambulizi ya kila aina, ndani ya vyama vya siasa, baina ya viongozi wa kisiasa, vyama vya upinzani dhidi ya chama tawala, nk.
Nani (Chama cha Siasa au Mwanasiasa) ataibuka mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huo ndio hoja ya bandiko hili, hasa kuhusu nafasi ya vyama vya upinzani.
Misingi wa bandiko hili ni kama ifuatavyo:
1) Viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa, katika kipindi chote cha miaka 5 ya utawala wa sasa, wakiishutumu Serikali kwa kile wanachodai kunyimwa haki ya kuendesha siasa, ambao ndio wajibu wa demokrasia ya vyama vingi.
2) Baadhi ya viongozi wa upinzani, si tu hawaridhishwi na jinsi na mwenendo wa Serikali kuhusu maendeleo na hasa uchumi, lakini wamekuwa wakimshutumu Rais Magufuli kwa maamuzi yake (ambayo wanaamini ni yake binafsi), km Kuzuia mikutano ya kisiasa, Ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato, Ununuzi wa ndege tena kwa pesa taslimu, Ujenzi wa miundo mbinu kwa fedha ya ndani nk.
3) Viongozi wa upinzani wamekuwa wakiishutumu Serikali, hasa Rais Magufuli (amri kutoka juu), kuhusika na matukio ya utekwaji, mashambulizi na kamatakamata ya viongozi wa vyama vya siasa kwa kile wanachodai ni sababu za kisiasa na utawala wa kidikteta.
4) Madai dhidi ya Serikali kwa utawala unaovunja Katiba ya JMT (km uhuru na haki ya kujieleza) na kutokuwepo Tume huru ya Uchaguzi.
5) Shutuma dhidi ya Msajiri wa vyama Siasa kutokana marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, 2012 inayompa madaraka makubwa.
6) Ndani ya vyama vya upinzani kumekuwepo na upinzani, shutuma za uongozi mbovu, na tuhuma za matumizi mabaya ya rasimali za chama.
7) Upinzani ndani ya vyama vya siasa ukafikia kiwango cha kufukuzana uwanachama na wengine kuhama vyama vyao kujiunga na vyama vingine.
8) Kumekuwa na maagizo na amri za viongozi wakuu wa baadhi ya vyama kwa matukio makubwa ya kitaifa km kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na namna ya kukabiliana na maambukizi ya COVID-19.
Hayo ni baadhi tu ya matukio yaliyojiri katika kipindi cha utawala wa Serikali ya awamu ya tano ambayo inajinasibu kuwa ya wanyonge. Baadhi ya mafanikio ambayo viongozi wake, na wa Chama wanadai ni utekelezaji wa yale yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi, 2015 iliyokiingiza chama madarakani. Wanadai kuwa utekelezaji wa Ilani hiyo, kwa kiwango cha juu, kunakipa chama nguvu ya kurudi kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi.
Katika mazingira mawili hayo ya kisiasa, yanayotofautiana kwa mbali, wapiga kura wataamini chama gani cha siasa na wagombea wake?
Nawasilisha