Baraka Sabi
Member
- Mar 16, 2017
- 19
- 14
Ni kawaida mtu anayeomba kuwa Mwakilishi wa watu hutumia lugha ya ushawishi kwa lengo la kutafuta imani toka kwa watu anaotaka kuwaongoza. Huu ndio uhalisia kwa mujibu wa sheria na taratibu zetu za nchi.
Cha kushangaza, wagombea walio wengi wamekuwa wakiwashawishi wapiga kura wao kuamini hata ahadi zisizoweza kutekelezeka ili tu wachaguliwe. Huu ni utapeli kama ulivyo utapeli mwingine wa kuwalaghai wavujajasho kuweka rehani maisha yao pasipo mafanikio wala ndoto ya kuyafikia maisha Bora. Ni hatari kwa Serikali kujaza watu wa kaliba hii kuongoza mihimili muhimu inayoshikilia Roho ya maendeleo ya nchi. Ni ngumu kupiga hatua kimaendeleo kwani tumeamua dira ya nchi imilikiwe na matapeli.
Nitoe wito kwa Viongozi mliokuwa madarakani, kamwe msifurahie kumaliza ungwe ya kwanza na kuomba ridhaa kwa mara nyingine. Jipimeni kama mlizitendea haki ahadi mlizowaahidi wapiga kura wenu (Kila mtu anakumbuka alichokisema). Kama sivyo, huna sababu ya kuendelea kuwafanyia usanii watu wenye kiu na njaa ya maisha Bora. Unga mkono jitihada za watu wenye uchungu na maendeleo na Mungu atakubariki.
Pia nitoe rai kwa mwananchi, uamuzi unaokwenda kuufanya October 2020, ndiyo sura ya maisha utakayoishi kwa miaka mitano ijayo. Baadhi ya watu wamekuwa wakijutia maamuzi ya chaguzi zao lakini kila uchaguzi unapokaribia hujitoa ufahamu na kujiripua tena. Kuwaweka madarakani wadukuzi wa maendeleo yetu ni ufinyu wa fikra.
Unataka Serikali ipi ikuletee maendeleo wakati Serikali yako uliyoiweka madarakani ni ya hovyo na isiyokuwa na uchungu na wewe? Tumwombe sana Mungu atuongoze kufanya maamuzi sahihi. Maamuzi yetu kamwe yasitawaliwe na ushabiki wa aina yoyote ile. Vinginevyo tutaimba sana maisha bora wakati misingi tunayoijenga ni potelea mbali.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"