Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Inadaiwa wagombea wote wa CHADEMA Jimbo la Serengeti mkoani Mara wameenguliwa.
Tutarajie ya mwaka 2019?
Kupata habari za kimkoa kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bofya hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
====
Kupitia mitandao ya kijamii, hususan X (zamani Twitter), viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameendelea kutoa malalamiko kuhusu kutoteuliwa kwa wagombea wao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji, na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Jambo TV imefuatilia sakata hilo kwa undani kwa kuzungumza na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Serengeti, Mossy Manawa, ambaye amesema kuna changamoto kubwa katika kata nne za Natta, Nyansurura, Magange, na Isenye.
Kwa mujibu wa Manawa, wagombea wa CHADEMA katika kata ya Natta wameambiwa kuwa chama chao hakitambuliki rasmi. Amesema, "Kama katika Natta chama hakitambuliki, sasa kilichowatambulisha wagombea katika kata hizi nyingine ni nini?"
Aidha, kwa kata za Isenye, Nyansurura, na Magange, Manawa alidai wagombea wamekumbana na madai kuwa muhuri walioutumia haukuwa sahihi, ingawa alisisitiza kuwa muhuri huo ni uleule unaotumika katika maeneo mengine yote.
Jambo TV imemtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Serengeti, Maulid Madeni, ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi, ili kutoa ufafanuzi juu ya changamoto hizo. Hata hivyo, juhudi hizo ziligonga mwamba, kwani baada ya mwandishi wetu kujitambulisha, Madeni alikata simu. Pia, hakujibu ujumbe wa maandishi (SMS) alipotumiwa kwa ajili ya maelezo zaidi.