Kuelekea uchumi wa viwanda: je, mikakati ni sahihi?

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Takwimu za kiuchumi zinaonesha kwamba 28.2% ya Watanzania ni maskini hasa wa vijijini ambao ni 75% ya hao (au 21.2% ya Watanzania). Ili kuendelea kupambana na changamoto hizo za kiuchumi, Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa 2015, ambayo ndiyo dira ya utekelezaji ya Serikali yake, chini ya Rais Magufuli, imeweka kipaumbele kukuza na kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vilivyo na uwezo wa kuajiri watu wengi na vyenye kuzalisha bidhaa zinazotumiwa na watu wengi wa ndani ya nchi na zile za kuuza nchi za nje.

Neno viwanda uhusu mabadiliko ya miundo/mifumo na/au mikakati ya maendeleo kutoka uchumi wa kilimo kwenda wa viwanda, ambayo huwa ni changamoto kwa nchi ambazo zinaendelea.

Je, mikakati na mipango yetu ya maendeleo inatupeleka huko?

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2018/19), uliotolewa Bungeni wiki hii, umeibua mjadala mkubwa tu ndani na nje ya Bunge na hata humu jamvini.

Mimi, japo si mtaalamu wa uchumi na ingawa nimeguswa na michango ya Wabunge watatu, ambao nimeweka hotuba zao hapa chini, kuhusu Mpango huo, kuna mambo ya msingi ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda, ambayo Waheshimiwa wabunge wanapaswa kuyazingatia.

Tafiti zinaonesha kwamba ujenzi wa viwanda huenda kasi katika nchi zenye: (i) msingi hafifu na isio endelevu ya viwanda (low industrial base); (ii) mikakati ya maendeleo inayoruhusu na kukuza soko huria (trade openness); na (iii) kukuza elimu na ujuzi (knowledge and skills accumulation) stahiki katika sekta za uchumi.

Ukisoma Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2018/19), kwa juu juu, bila kuuhusisha na Mipango/Mikakati ya maendeleo iliyopo, hakika utahitimisha kwamba mwelekeo wetu kwenye uchumi wa viwanda siyo sahihi.

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2018/19 ni mwendelezo wa mikakati ya Serikali kujenga kwanza uchumi wa kujitegemea:
i) Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (Agricultural Sector Development Programme - ASDP II).
ii) Kuiendeleza Sekta ya Mifugo na Uvuvi
iii) Kuhakikisha kuwa Sekta ya Maliasili inapewa msukumo wa kutosha ili iweze kuchangia kikamilifu katika kubpresha maisha ya wananchi.
iv) Kukamilisha Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu (2010/20).

Mipango na mikakati hiyo ni mwelekeo tu wa kutekeleza na kuweka nguvu kubwa kukamilisha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16 - 2020/21).

Swali la msingi la kujiuliza hapa ni: Je, tunaanzia wapi, kama nchi?

Ujenzi na ukuaji wa viwanda unaenda sambamba na maendeleo ya kilimo. Kwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania maskini wako vijijini, na shughuli kubwa ya kimaendeleo ni kilimo na ufugaji, ujenzi wa viwanda utaweka msukumo kukua kwa sekta.

Kufanikiwa hayo, ni pale tu Serikali itaweza kukusanya kila kodi, wakati huo huo pato hilo likatumika kuimarisha na kuboresha vichocheo muhimu vya uchumi km miundo mbinu (usafirishaji) na huduma za jamii (elimu na afya).

Waheshimiwa Wabunge na wanajamii humu, wanaijua Tanzania kabla ya uhuru na baada ya uhuru, lakini hatujajiweka tayari kujenga Tanzania mpya. Bado tunataka kuendesha maisha yetu kimazoea (business as usual).

Nikirejea kaulimbiu ya Rais magufuli HapaKazi tu, bado Watanzania, hasa Wabunge wawakilishi wetu, hawajaielewa na ndiyo maana bado wana mawazo ya kinadharia - uchumi wa vitabuni.

HapaKazi tu ni nadharia mpya ya kiungozi, kiutawala na kiuchumi ambayo msingi wake mkuu ni Malengo Makubwa na Utekelezaji Makini. Na ndicho tunachokishuhudia sasa hivi Tanzania ikielekea kwenye uchumi wa viwanda.
 
Kweli kabisa CCM wanatupeleka pabaya.
Hutofautiani na hao Wabunge kwa sababu ya mawazo ya 'business as usual'.

Siyo rahisi kuelewa na kukubali kuwa hatua za kukuza uchumi, zinatekelezwa sasa, ni sahihi kama utazichambua kwa mtazamo wa kisiasa.

Moja ya misingi mikuu ya maendeleo ni Uongozi bora kwa kusimamia rasmali watu, ardhi na kutekeleza sera kwa uthubutu na utashi wa kisiasa.

Ukiwasikiliza hao Wabunge wote, hasa Mh Mbowe, hakuna anayepinga kuwa CCM ina sera mbaya za uchumi. Wote wanadai utekelezaji mbovu na kwamba wateule wake Rais wanamwangusha kwa kumdanganya.

Rais Magufuli anadanganyika kweli? Kwamba anakubali kupokea takwimu za uchumi zilizopikwa!! Si kweli na si kweli kabisa! Ushahidi ni hatua za papo kwa papo anazozichukua dhidi ya wateule wake wanaomwongopea.

HAPA KAZITU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…