Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Kama vile ilivyo bandwidth yaani capacity ya watu kuweza kuongea kwa wakati mmoja kwenye simu / mitandao ndio hivyo Umeme ukishauzalisha inabidi utumike, sababu kuutunza ni gharama, (Ingawa unaweza kutumia Bwawa kama Battery), kwahio nikichukulia mfano wa kama watu wanaweza kunywa maji Pipa moja nyakati za mchana na wewe unazalisha pipa moja ni kwamba mchana itakuwa peak time ingawa usiku huenda ukawa na ziada, ambayo isipotumika inapotea; Kwahio ziada hio hata ukiuza kwa bei ndogo Offpeak (bado ni nafuu kwako); Na kama unaweza kuzalisha Pipa mbili basi ni bora yale maji usiyanywe tu bali uyatumie kuongea sababu kuna Pipa zima litakuwa linapotea bure (hivyo kama tuna ziada ni bora bei ikashuka watu watumie Umeme kupikia)
Ni Vema tukawa Connected na Majirani Wote
Kama mwisho wa siku plan yetu ni kuuza mpaka nje ni vema tukawa connected na majirani ili ile ziada tukaweza kuuza au kama wao wakiwa na ziada tukaweza kuchukua iwapo tu itakuwa gharama ndogo kuliko tuliyonayo
Kuongeza Matumizi ni Kushusha Bei
Tanzania sio kwamba tuna ziada, bali katika matumizi watu wanajinyima kutokana na gharama (units za umeme sio affordable kulingana na kipato cha mtu) hata ile Tariff Zero (Tshs. 100 kwa Unit) Mijini imefutwa na kama ndugu zetu wa Kaskazini umeme utanunuliwa nje kwa gharama ambayo ni zaidi ya hio Tshs 100/= ni vigumu kuwauzia chini ya hapo. Na kama tunapanga kuuza nje kwanini tusiwekeze ifike Kaskazini ili ziada nyingine iende Kenya. Kununua tununue tu iwapo itakuwa gharama nafuu (Na mpaka sasa bei za Units zilizopo sio Nafuu hata kidogo); Kama kabla ya Bwawa na baada ya Bwawa bei hazishuki kwanini tulihangaika kutengeneza Mradi ?
Tujenge Miundombinu ya UMMA na Sio watu Binafsi Kina ADANI (Sababu tukiweka mtu Binafsi anayetaka Faida na Umeme utapanda); Watu Binafsi Wazalishe iwapo wataweza kutupa Bei chini au Sawa na Inayozalishwa na UMMA
Tusifanye kosa la kuwapa watu binafsi (Profit Oriented) kwenye hii Huduma sababu mwisho wa siku ni mwananchi apate umeme affordable, mtu binafsi atataka profit na katika ile profit lazima itoke kwa mtumiaji hivyo ni vema miundombinu (Distribution) ikafanywa na UMMA / Serikali lakini Uzalishaji akafanya mtu yoyote binafsi kama tu ataweza kuuza bei ambayo ni ya chini kuliko iliyopo / inayoweza kuzalishwa na Tanesco kwa kipindi husika.
Nishati ni UHAI makosa yanayofanyika leo yatalicost Taifa karne zijazo kama vile Makosa ya kina DOWANS yanavyolitafuna taifa mpaka Kesho...