Philipo Mwakibinga
Senior Member
- May 13, 2013
- 110
- 175
Na Philipo Mwakibinga
Rais Mama samia amedhihiri kuwa anataka Tanzania yenye kiwango kikubwa cha Demokrasia, ambacho kinapimika kwenye viwango vya Kimataifa.
Badala ya kujifanya hatujamuelewa sasa tumsaidie ili Tanzania ya Wote iwezekutamalaki. Niwakati muafaka wa kilammoja wetu kujivunia hili na kuanza kuliimba kwavitendo bila husda yoyote.
Tanzania ya Mama Samia itaweza hata kuwa na Bunge lenye meno kama lile la Samuel Sitta tujipe muda maana wakati ni Mwalimu mwenye weledi wake. Tanzania ya Mama Samia ipo siku itatoa Spika wa Bunge kutoka Upinzani na Naibu wake kutoka CCM inawezekana kama tutamsaidia mama kuhakikisha Demokrasia hii anayoirejesha na kuikuza itawekwa kwenye KATIBA.
Mama siyo mtu wa makundi na minyukano ya kisiasa isiyo na tija, mama siyo muumini wa mapambio na ngonjera za kumsifia kwa woga na jicho la ngebe wakati moyo wako hautaki. Mama anapenda mtu anayeuishi msimamo na ukweli wake wa moyo.
Ndiyo maana hata teuzi zake zimesadifu hayo. Mama ni mtu anayetaka usiyabatize mabaya yako kwa mazuri uliyonayo, anataka mazuri yawe mazuri yapewe nafasi na kwa uzitouleule mabaya nayo yashughulikiwe kikamilifu kwa kufuata misingi ya haki na usawa.
Kuna watu wanaweza wasimuelewe mama hasa kutokana na maisha waliyoyatumikia zama fulani lakini ukweli ni kuwa mama atapendwa na wote wawe marafiki au maadui tulioumizana zama zile. Hii inatokana na mama kuwa mponyaji wa majeraha na makovu ya madonda na matone ya machozi katika dhamira za baadhi ya wenzetu.
Pamoja