Kuendelea na shughuli zao za kawaida je Watanzania wamekubaliana na Rais wao!?

Kuendelea na shughuli zao za kawaida je Watanzania wamekubaliana na Rais wao!?

Hata Sina kinyongo

Senior Member
Joined
May 16, 2020
Posts
118
Reaction score
280
Pamoja na janga la Covid 19 kuendelea kuukumba Ulimwengu na karibu Nchi nyingi kuwafungia wananchi wao lakini hali ni tofauti kwa upande wa baadhi ya mataifa ikiwa pamoja na Tanzania.

Watanzania wengi wameendelea na shughuli zao za kawaida kama wanavyoaswa na Rais wao na inaonyesha hawana munkari wala muhali kwalo.

Je, kwa muktadha huo ndiposa watanzania wapo pamoja na Rais wao!?
 
Unakuta mtu huku mitandaoni anamkosoa Magufuli kwa kutoweka lockdown ila na yeye huku mtaani anajichanganya na watu kama kawaida akiendelea na shughuli zake.
 
Hili swala bado lipo fifty fifty, hakuna nchi inayoweza kujinadi kwamba lock down kwao imetoa ufumbuzi kwa 100%.
 
ukichunguza wanallilia lockdown ni wale wafanyakazi waajiriwa wavivu wa mwili mpaka akili wanaodhani wakikaa nyumbani wataendelea kulipwa kama marekani na uingereza.
 
Anaye lilia lock down mchunguze sana. Ana kaakiba kake labda ka kuweza kununua chakula cha kumtosha aweke ndani ale kwa uchoyo huku akikaanga kitunguu majirani wasikie harufu. Ukifika akuambie kuwa serekali ya JPM ndiyo inakutesa lau uichukie. Hiyo lock down kwa mnyonge huyu unategemea akae ndani siku ngapi? Wengi tunategemea kuuza maparachichi tununue unga umfungie mtu huyo ni sawa?? Tulieni tu JPM mtampenda soon
 
Vipimo tumeambiwa vibovu vinatoa majibu positive mpaka kwa mapapai, then mtu huyo huyo aliesema hivyo anaibuka na kusema maambukizi yamepungua, amejuaje? kwa majibu ya vipimo gani?!

Vipi kama watu wameamua kukaa na wagonjwa wao nyumbani kwa sababu hospitalini vipimo vibovu, hivyo hawaoni sababu ya kwenda hospitali...

Ule uchunguzi wa vipimo mbona majibu bado mpaka leo?

Vipi siku hizi mbona hatupewi taarifa kuhusu Corona na waziri husika, ili hata kama ni kweli maambukizi yamepungua tujue mapema, na sio kusubiri mpaka Rais alete taarifa? au kamzuia waziri kutoa taarifa, if yes; anataka kujimilikisha hii issue kwa manufaa ya nani?

Halafu at the middle of all this, anatokea mtu anasema anafikiria kufungua vyuo!.

Naona bado kuna utani mwingi kwenye hii issue serious ya Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili swala bado lipo fifty fifty, hakuna nchi inayoweza kujinadi kwamba lock down kwao imetoa ufumbuzi kwa 100%.
Acha uongo wewe...


But the coronavirus crisis has made Mr. DeWine something that decades in elected offices never did: a household name. A Republican, he took early and bold actions to lock down his state, even as the head of his party, President Trump, dismissed the threat of the pandemic.

Mr. DeWine’s decisiveness — closing schools before any governor in the country, postponing the state’s March 17 primary election to protect voters — sent his popularity soaring. The folksy governor, previously best known for an annual ice cream social at his rural home, became something of a cult figure on social media. Ohioans tuned into his five-day-a-week briefings to celebrate “Wine With DeWine,” a ritual whose motto is “It’s 2 o’clock somewhere.”
 
Back
Top Bottom