Uchaguzi 2020 Kuepuka rushwa wakati wa kampeni basi kusiwepo Uchaguzi, rushwa haiepukiki na Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Kuepuka rushwa wakati wa kampeni basi kusiwepo Uchaguzi, rushwa haiepukiki na Uchaguzi

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Bora kipengele cha rushwa wakati wa uchaguzi kiondolewe tu yani iwe free mtu kufanya atakalo kushawishi watu wamchague.

Kwa sababu lengo la rushwa ni kushawishi jambo huyu mtoa rushwa alipate hilo jambo. Sasa manake rushwa lengo lake ni ushawishi.

Kwa hiyo ukitoa pesa wakati wa kampeni ni rushwa kwa sababu inashawishi. Ukitoa maneno mazuri wakati wa kampeni ni rushwa kwa sababu unashawishi.

Ukitoa kanga na vitenge ni rushwa kwa sababu unashawishi. Ukitoa chakula ni rushwa kwa sababu unashawishi. Ukitoa shoo kali kupitia wasanii ni rushwa kwa sababu inashawishi.

Hatuwezi tukaipinga rushwa kwa jina lake wakati huo kwa namna yake na mtindo yanaingia mambo mengi yenye sifa ya rushwa.

Wakati pesa,vyakula na nguo vinaweza kuhisabika kama ni rushwa kwa sababu ya ile maana na malengo yake ni ushawishi basi ndivyo hivyo hata ahadi za maneno nzuri kwa wananchi na kutumia wasanii pia haya yanashawishi watu kumchagua mfanyaji hayo mambo.

Kwa hiyo kama tunapinga rushwa basi tupinge ushawishi wowote wakati wa kampeni utakaotumika kuwavutia watu.

Haiwezekani tuibague pesa na chakula tuite rushwa lakini mambo mengine kama kutumia wasanii na KUTOA ahadi nzuri zisiwe rushwa,pesa ina dhambi gani mpaka ibaguliwe hivi ?

Sasa eidha waruhusu ushawishi wa jamna yeyote utakaotumika kumchagua mtu Au wakataze kampeni kabisa iwe inatangazwa tu kuwa uchaguzi ni tarehe fulani,hii pia inayoitwa rushwa rushwa itakuwepo .

Au kusiwepo na uchaguzi kabisa wa kuchaguliwa na wanachi kwa sababu rushwa inakuwa inatapakaa kila kona.
 
Back
Top Bottom