Kufa kwa biashara ndogo ndogo Tatizo ni nini?

Kufa kwa biashara ndogo ndogo Tatizo ni nini?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Kwa kawaida mtu anapoanza biashara yoyte,kubwa ama ndogo huwa anakuwa na malengo fulani.Inapotokea biashara hii imekufa au kufungwa huwa pia kuna sababu.

Kwa utafiti mdogo niliofanya kumekuwa na kasi kubwa ya ufaji wa biashara na hii sio kipindi hiki tu bali hata vipindi vya nyuma ingawa kasi ya kipindi hiki imezidi kidogo.Ukitaka kutambua hili jaribu kupita katika maeneo uone namna ambavyo ukipita eneo fulani unakuta biashara zinabadilika ndani ya kipindi kifupi.

Hili limenifanya nijiulize maswali mengi ikiwamo Je kufa huku ni kwa sababu gani?

Tujadili hapa kwa pamoja je chanzo ni biashara kuwa ngumu,kukosa ujuzi wa uendeshaji ama ni watu kupata fursa nyingine na kuamua kuacha biashara husika

Tujadili kwa ajili ya kupeana elimu na ujuzi na uzoefu.
 
Nadhani sababu mojawapo ya biashara ndogo kufa ni kukosa ubunifu na hivyo kushindwa kumudu ushindani mkubwa uliopo sokoni.
 
Biashara ndogo huwa hazina pesa yakutosha kuendesha biashara ndio maana zinakufa hasara zinapotokea, napekee yakujinusuru na hili nikupunguza gharama za uendeshaji na kukuza njia zaidi ya moja za mapato.

Zinaweza vipi kupunguza gharama za uendeshaji?
IT/TEHAMA. Biashara ndogondogo inabidi zitumie zaidi utaalamu au wataalamu wa ICT(TEHAMA) ilikupunguza gharama za uendeshaji.
Mfano: mfanyabiashara mdogo anapambana kutafuta kuweka biashara yake sehemu zenye wapita njia wengi ambapo sehemu hizi ni ghari sana kuzimudu, kumbe angeweza tu kujitangaza kwenye mitandao yakijamii, akafungua blog au website kuhusu biasharae yake, akauza bidhaa zake kwenye mitandao mengine kama alibaba,ebay, jumia,zoomtanzania,kupatana,amazon n.k

Ukiangalia kumbe mtu anaweza kuwa na duka lake tu huko mtaani mafichoni na akawa na wateja wengi mno kishinda ata yule aliyoko njia panda.

Gharama zingine unazowezakupunguza ni kutunza taarifa, watu wanaandika kwenye vitabu vinaliwa na panya,vinachanika, gharama za kuprint. Kumbe angeweza kuwa na tablet yake tu au smartphone akapakua app kama SKYMKOBA ukatunza kumbukumbu za mauzo,matumizi kiurahisi kabsa na app nyingine nyingi za bure zinasaidia wafanyabiashara kwenye kutunza kumbukumbu, pia kuna app zinatengeneza invoice, kuna app kama Nala unafanya miamala nakumbuku zinatunzwa, namambo mengine mengi yanaweza kusaidiwa na TEHAMA(ICT) ilikusudi biashara zisifungwe.

Unapo sikia soko la nje au soko lakitaifa, huwezi kulifikia bila internet na watu wa IT internet inachukua sehemu kubwa ya masomo yao huko chuoni kama ulikua hujui, ndio maana hawa watu wa IT ni msaada wa biashara ndogondogo kujiendesha bila kutumia gharama kubwa.
 
Duniani 30% ya biashara zinazoanzishwa hufeli miaka miwili baada ya kufunguliwa
Baada ya miaka mitano hufika 50%
Baada ya miaka 10 hapo hufika 66% ya biashara kufungasha
Na sababu zipo nyingi tu
 
Mtazamo wangu
Mo

Kwa kuwa bihashara ndogo nyingi zinamilikuwa.na.mtu moja, moja ya mtaji muhimu ni afya ya mmiliki na muda wake, kwa hiyo chochite kitakachoathiri hayo mawili kinaweza kuwa chanzo.cha.kudorora kwa bihashara na hata kufa
 
Pia kutegemea sana mapato ya bihashara hiyo kusolve kila kitu chako hasa kwa bihashara inayoanza inaweza kuwa sababu pia
 
Write your reply...Sababu in nyingi zinzochangia kufa kwa biashara Tz na duniani.#1 Afya in jambo muhimu sn ktk ukuaji was biashara mahari popote-watu wako rafu na afya zao hasa nyakati ambapo kipato kinaongezeka.#2Nidhamu ktk matumizi ya pesa .#3Kukosa elimu ya ujasiliamali na biashara yaani watu wanafanya mambo kwa mazoea nk.#4 Biashara yoyote inahitaji uvumilivu bila kujari Leo umepata au umekosa.#5.Malengo-wengi hawana malengo ktk biashara zao wanafanya kwa kushindana na Fulani au km Jirani au na yy wanafanya ili aonekane yupo ktk biashara
 
Wengi wamezungumza, kufa kwa biashara ndogo naona zaidi ni;
1.kukosa uaminifu katika jamii zetu, mfano wa hili nauona katika biashara yangu ya pilipili watu wengi ikiwemo uauza chips huamini biadhaa kubwa na kukosa imani na local products.

2.Kukosa support kutoka katika family au watu wako wa karibu wanaokuzunguka, mfano mimi ni mjasilia mali mdogo no support kutoka home wanaona kama haiwezekani tu, so kwa mtu mwenye moyo mwepesi huwezi move kabisa.

3.Bei na Branding( I guess)
 
Ni mjasiriamali na nina uzoefu mkubwa na biashara ndogo.Kwanza ni tabia ya kuanzisha biashara kwa kuiga.Pili ni uridhika haraka kiasi ambacho hata kuipa facelifting biashara yao hufanyi na la tatu ambalo ndio kubwa hasa ni NIDHAMU YA UWEKAJI NA MATUMIZI YA PESA.Hapa tunachemka mno na ndipo panatuumiza.Binafsi nimeamua kuweka mapato yangu ya kila siku TIGO pesa kama uthibiti lakini bado kuna wakati natumia isivyostahili.
 
Sehemu .yabiashara ilipo.kukosa wateja . Kufanya mtaji huohuo kua kiinua mgongo maana yake kula hapo hapo lazima biashara iyumbe huu mfano tu
 
Hapa kwenye Afya umenikumbusha kitu,kuna Boss wangu mmoja hivi wa zamani jamaa ni Bilionea na ni mtu wa mazoezi japo umri wake ni above 50 years na hata akiwa kazini hali chakula chochote zaidi ya chakula cha kutoka nyumbani kwake yaani hata kama kazini kuna canteen hagusi chakula chenu na hakiamini hicho mtakula wenyewe.
Kwa hiyo kama yupo bize kazini na hana muda wa kwenda kazini atapiga simu nyumbani waandae chakula akabidhiwe dereva wake au mkewe apakie kwenye gari kiletwe ofisini kwake.
Ila watu wa kawaida huwa hatujali tunakula hovyo tu kwenye mgahawa wowote tunaagiza tu chakula
 
Una uza nini? Naje ume wasoma vipi washindani wako na kushindani nako!!
UnakoEnda kununua bidhaa ndiko pata Amua upate faida kiasi gani? Na wateja utapata wengi kiasi gani.
 
Back
Top Bottom