Kufa upendwe,ukiwa hai pita kushoto

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Habari wanajamvi

Bila kupoteza muda naomba niwaeleze mtu anapokufa ndo anakuwa mzuri na ndo lugha za huruma hutolewa "NINGE NINGE NINGE" zinakuwa nyingi lakini wakati akiwa hai hakuna msaada uliowahi kutolewa

Watu sasa hivi wanajinyonga kwa ugumu wa maisha au matatizo ya kisaikolojia

Ugumu wa maisha
Huyu mtu huenda akapata wakati mgumu sana katika maisha,ila mitaa aliyopo kuna watu na ana ndugu na huenda aliwaomba msaada kumsaidia ili apite katika wakati mgumu unao mkabili lakini ndugu,jamaa na marafiki,na majirani wakasema kila mtu apambane na hali yake

Siku huyo mtu akijinyonga baada kushindwa kuhimili mikikimiki ya hapa duniani ndipo majirani,ndugu,marafiki hujitokeza na kusema si angelisema asaidiwe kuliko kujinyonga,hapo ndo utajua BINADAMU NI WANAFIKI,kufa upendwe

Matatizo ya kisaikolojia

Huenda imesababishwa na mapenzi au biashara kuyumba na kupata hasara kubwa kwa wale matajiri

Kila mtu ana rafiki hata kama wewe ni mbaya sana lakini lazima uwe na rafiki,mtu huyu anapopata tatizo marafiki hupata taarifa mapema na wengine hupuzia kumsaidia ,likitokea ndo unamuona anakuja anasema " SI ANGALISEMA" kumbe ana taarifa

RPC Geita ,sio kwamba wanaojinyonga hawatoi taarifa juu ya matatizo yao,wanasema sana ila binadamu tumekuwa wabaya sana
 
Mtoa Mada Kama Tako Unalo Mi Nitakupenda Ukiwa Hai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…