GoJeVa
Member
- Sep 15, 2021
- 41
- 60
KUFAHAMIANA (CONNECTIONS) KATIKA KUPATA KAZI.
Kuna tabia imezuka sana katika jamii zetu na kadri tunavyosonga mbele inaelekea kuwa sugu, si nyingine tabia hii ni kupeana kazi/ajira kwa kufahamiana. Kwa lugha ya kiingereza tunaita CONNECTIONS. Katika andiko langu hili nitaangalia zaidi watu wenye taaluma na fani mbali mbali na harakati zao katika kupata kazi. Kwa kuanza nitasimulia simulizi yangu kwa kifupi na harakati zangu za kupata ajira baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo;
“……………baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo, niliingia mtaani kutafuta ajira. Kwa upande wangu nilichelewa kupata ajira na hata baada ya kupata kwenye moja ya sekta binafsi malipo hayakuwa mazuri hivyo nikaamua kufanya biashara ndogo ndogo, ila baadhi ya watu tuliomaliza nao chuo kama watano hivi ambao nilikuwa nao jirani walipata kazi kwenye sekta binafsi baada tuu ya kuhitimu chuo. Haikuwa ni kitu cha ajabu, kwani wengine hupata kazi kutokana na bahati zao, wengine uwezo wao wa kitaaluma na wengine kwa njia ya kufahamiana(connections). Hawa wenzetu watano walifanikiwa kupata ajira hizo kwa sababu walikuwa na ndugu zao katika sekta mbali mbali. Ilifika kipindi niliamua kuingia kwenye biashara za umachinga ambazo nazifanya hadi sasa, kwa sababu sikuwa na mtu mwenye nafasi ambaye nafahamiana nae…………………….”
Na ikumbukwe sio wote wanaopata nafasi kwa kujuana (connections), hawana sifa hapana wengine huwa ni mahiri na wana sifa nzuri.
Hebu sasa tujiulize maswali machache kuhusu suala hili;
*Je? Unaamini katika nchi uliyopo kuna tabia ya kupeana kazi kwa kujuana.
*Je? Wewe ni muhanga wa hili.
*Kama hili suala lipo, Je? Unashauri nini wahanga na jamii kwa ujumla.
Mimi kama mwandishi wa hili andiko, napenda kushauri kwa kila mmoja kuwa mahiri katika taaluma na fani yake kwanza, ndio uanze kutafuta kazi, haya mambo ya kupeana kazi kwa kujuana na kufahamiana tujifanye kama hatuyaoni. Namaanisha tusikose kazi kwa kukosa umahiri, bali tukose kazi kwa sababu zingine kama hizo za kukosa kufahamiana na watu wenye nafasi, nasema hivyo kwa sababu ni ngumu kulazimisha kujenga mahusiano na watu wenye nafasi kwenye sekta mbali mbali, ikumbukwe sijasema haiwezekani na kama inawezekana kujenga mahusiano (connections) na watu wenye nafasi zao basi fanya hivyo ila ni muhimu fanya hivyo bila kuuza UTU wako(ni ushauri). Kwa kumalizia tusome ushauri hapo chini;
*Tujishughulishe kwa bidii katika utafutaji wa riziki zetu, tujitume kadri ya uwezo wetu ila tuu tusivuke hatua itakayopelekea kuhudharirisha UTU wetu. Katika utafutaji wetu tuwe na KIASI. Tukilinda utu wetu itasaidia hata pale tukipata mafanikio tufurahie mafanikio yetu bila kujutia wala kulaumu, tukumbuke radha ya maisha ni furaha.

Upvote
3