Kufanana kwa Wanaowanyanyapaa kina Mwabukusi na visa vya Yesu

Kufanana kwa Wanaowanyanyapaa kina Mwabukusi na visa vya Yesu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kina Mwabukusi na wenzake wametokea na inayoaminika kuwa ni agenda muarobaini wa matatizo yetu ya muda mrefu kama nchi:

"Kupambana na maadui zetu kwa vitendo."

Haipo siri kuwa hii itatuvusha, na hatimaye ushindi ni dhahiri.

"Kwani ni lini maneno matupu hata yalipata kuvunja mfupa?"

Ajabu na kweli kuna wenzetu wamechukia na kufura kwa hasira kali kuliko hata za maadui zetu. Kwamba wameshindwa hata kukaa kimya tu.

Misahafu inawatambua vyema watu wa aina hii:

1. Kisa cha tajiri kijana (Mt. 19:16-24):

.... 21 Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. ...


2. Kisa cha mwana mpotevu (Lk. 15:11-32):

.... 28. Yule kaka akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akaenda nje akaanza kumbembeleza. 29 Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Angalia, miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana mbuzi ili nisherehekee na marafiki zangu. 30 1Lakini huyu mwanao ambaye ametapanya mali yako kwa makahaba amerudi nyumbani nawe umemchinjia ndama aliyenona!’

Kwa hakika ukombozi wa nchi (si lelemama) kama (tu) asemavyo nabii Issa kuhusu kuingia mbinguni:

"Kwamba, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano ...."

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Aluta continua!
 
Adui mbaya, hatoki mbali, ni yule mtu wa karibu nyumbani mwake.
 
Back
Top Bottom