Wawili hawa ni majaji ambao wote wameshughulika na kesi inayomhusu Mh. Mbowe na wenzake.
Wote ni wateuliwa mahiri wa hayati Magufuli. Wote kwa maamuzi yao wameuacha ulimwengu wa haki ukiwa umepigwa butwaa.
Kwa hakika hawajaonekana hadharani wenye kuyafagilia kwa dhati yao, maamuzi yoyote ya wawili hawa.
Haijulikani kama wote watadumu na kesi hii hadi mwisho.
Wakati Siyani alikuwa ni mswalihina ustaadhi wa swala tano (tukipisha adhana muda ukitimu), japo yeye alizingatia muda. Kwake saa tatu yake ilikuwa saa tatu kweli. Baada ya dakika 10 yake ilikuwa kweli baada ya muda huo.
Tofauti na hapo, leo ya Tiganga inaweza kumaanisha kesho vile vile na bila hata ya neno la samahani. Akisema saa tatu ujue saa nne au hata saa tano. Kwake huyu saa au muda hauna maana.
Siyani mahakamani alikuwa na authority japo yenye kuashiria uwezekano wa haki kutendeka.
Hakukuwa na mzaha mzaha wa mashahidi kuthubutu hata kutupia au kupiga chabo. Sasa Tiganga.
Yote kwa yote wawili hawa kwenye kuuma na kupuliza au kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa - wako vizuri (au kama asemavyo beberu -- wake perfect)!