Kufanikiwa katika maisha sio elimu tu, bali na ujasiri wa kujiamini na kuthubutu!

Void ab initio

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
5,720
Reaction score
5,659
[emoji144][emoji404][emoji383]⚙[emoji144][emoji404]

KUFANIKIWA KATIKA MAISHA SIO ELIMU TU, BALI NA UJASIRI WA KUJIAMINI NA KUTHUBUTU!

[emoji116][emoji116][emoji116]
Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

[emoji539][emoji591][emoji436] Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

[emoji144][emoji432] Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi [emoji537] na [emoji594] magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!).

Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

[emoji144][emoji404] Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

Hii inachangiwa na mambo mawili.

1⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli.

Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio.

Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

2⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani.

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze.
 
Kabisa,na Kubwa zaidi Elimu yetu imekaririwa Tu jambo ambalo halimpi MTU nafasi ya kujitandaza ndio maana naamini awamu hii itafumua kabisa mfumo huo
 
Itakuwa hayo magari yanatengenezwa na ambao si wasomi na hayo majumba yatakuwa yanajengwa na wasiosoma ndo maana yanamilikiwa sana na wasiosoma.

Hebu fikiria kama dunia ingekuwa imejaa wasomi tu au matajiri tu, HALI INGEKUWAJE?? Hebu fikiria kama vidole vyako vingekuwa vyote ni GUMBA??????

NDO MAANA KUNA UKUTA NA KUNA MSINGI. Ukuta ukijidai unadhibitiwa faster na msingi.

Uwepo wa tofauti kadha wa kadha ndio unaofanya TUHESHIMIANE maana kila mmoja anamhitaji mwenzake.
 
Unajua elimu ya Mohamed Dewji na Reginald Mengi? Acheni kutetea uvivu wa kwenda shule. Kwani kuna dhambi gani kuwa tajiri na huku umesoma?
 
Umeongea vizuri, ila katika suala la mitihani, ambapo unapimwa uwezo wa mtu kufikiri na kutatua jambo kwa haraka, unataka napo pawe na majadiliano? Hapana mkuu. Lakini mengine upo sawa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…