Kunyanyuka kwako kunakuja kwa kuwanyanyua wengine, usipambane sana kutoka wewe mwenyewe kwenye mzunguko wako, utarudishwa nyuma sana na kulalamikia sana wengine kwa sababu utaona wanafanyika mzigo kwako, lakini hebu jitahidi unaponyanyuka mshike mkono na mwingine/wengine mara nyingi uwezavyo, matokeo yake ni mazuri zaidi.
Wanainuana kwa kupeana nafasi za ajira na fursa, kwa watu wa mzunguko wao hivyo kwa aliefanikiwa utakuwa ameshawasaidia kupata kazi watu wengi ambao wako kwenye mzunguko wake wengi, hii inaweza kuwa moja kwa moja kwenye kazi yake ama sehemu nyingine alipoona fursa ipo ya mtu wake wa karibu kupata kipato zaidi.